Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Shirika la Ndege la Precision Air limezindua mpango maalumu  wa mafunzo kazini kwa ajili ya vijana wa Kitanzania wenye ndoto za kua wahandisi wa Ndege ili kukabiliana na uhaba wa wahandisi katika sekta ya anga nchini katika siku za usoni.

Shirika hilo limeanzisha mpango huo katika jitihada za kuendeleza rasilimali watu inayohitajika katika katika kitengo chake cha ufundi kupitia mafunzo maalumu kwa wanafunzi wa ufundi  pamoja na mpango wa mafunzo kazini na tayari limeajiri mafundi 22 kupitia mpango wa mafunzo kazini katika kitengo chake cha Uhandisi na ufundi na watakua wakifanya kazi huku wakiendelea na mafunzo ya vitendo. 

Akizungumzia mpango huo, Mkurugenzi Mkuu wa Precision Air, Sauda Rajab amesema, upatikanaji wa rasilimali watu katika sekta ya anga umekua changamoto kubwa nchini. Ameongeza kuwa Precision Air kama shirika lenye uzoefu haliwezi kubaki kulalamika na ndo sababu shirika limechukua hatua ya kuanzisha mpango huo ili kusaidia katika kutatua tatizo. 

“Tunajivunia mchango wetu katika kuendeleza rasilimali watu wenye ujuzi unaohitajika katika sekta ya anga Tanzania.Kupitia mpango wetu huu wa mafunzo kazini nimatumaini yetu tutaweza kutengeneza wahandisi wengi wa ndege ili kuweza kukidhi mahitaji ya soko na mahitaji yetu kama shirika,"amesema 

Kwa upande mwingine Sauda, ameeleza kuwa inachukua takribani miaka nane (8) kumuandaa Muhandisi kamili  mwenye leseni, huku pia ikigharimu fedha nyingi katika kusomesha wahandisi, hivyo anatarajia wadau wengine kwenye sekta ya anga watafanya jitihada kama za Precision Air, badala ya kutegemea wataalamu kutoka nje pekee, ili kuimarisha sekta na kutengeneza ajira nyingi zaidi kwa vijana wa Kitanzania.

Katika kutekeleza hilo Shirika la ndege la Precision Air pia lilisaini mkataba na Chuo cha Usafirashaji (NIT) mnamo mwaka 2017, mkataba unaowawezesha wanafunzi kutoka chuo hiko kupata nafasi za mafunzo ya vitendo kupitia shirika hilo na mpaka sasa wameshatoa mafunzo kwa wanafunzi 33.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...