Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa ameyataka makampuni ya uchimbaji visima kuomba vibali ili waweze kuchimba visima hivyo pamoja na ulipaji wa kodi ya utumiaji wa maji.

Hayo yamesemwa na Waziri leo alipokagua visima vya kampuni ya Winners Traders iliyochimba visima katika Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa na Uhuru Mchanganyiko Jijini Dar es Salaam.

Prof Mbarawa amesema kuwa jukumu la utoaji vibali la uchimbaji wa visima ni kutoka kwa Bonde la Wami Ruvu na ni lazima wakubaliwe kwa ajili ya kuendelea na shuguli zao za kuchimba wakiwa wamekamilika.

Amesema kuwa, makampuni mengi yamekuwa yanachimba visima bila kuwa na vibali na amewataka wamiliki wote kuanza kufuatilia vibali ili waweze kupewa haki ya uchimbaji ikiwemo na kulipa kodi ya kila mwaka kwa serikali.

"Awali katika Wilaya ya Temeke ukiwa unachimba kisima unatumia mita 40 unakuta maji ila sasa hivi unaweza kufika mita 90 ndio unakutana na maji hilo linatokana na uharibifu uliokuwa umefanywa na watu wasio waaminifu kuchimba pasipo kuwa na kibali kutoka kwa wahusika ambao ni Bonde la Wami Ruvu," amesema Prof Mbarawa.

Kwa upande Bonde la Wami Ruvu, Afisa Maji Wami Ruvu Simon Ngonyani amesema kuwa jukumu la utoaji vibali ni la kwao na utakapokuja kuomba lazima ulipie hicho kibali pamoja na ada ya kila mwaka, yapo makampuni waliyopewa na wengine hawajapewa tuliwakatalia ila wamekuwa wanaendelea kuchimba.

Ngonyani ametoa rai kuwa, wanawapa muda ili makampuni hayo yaende wenyewe kushughulikia vibali kwa wakati kabla hawajaanza kuwachukulia hatua kwani wamekuwa wanakwepa kulipa kodi kutokana na kuchimba visima kinyemela.

Prof Mbarawa amekuwa katika ziara maalumu ya kukagua miradi mbalimbali ya maji ikiwemo kwenye viwanda vinavyopata huduma za maji kutoka DAWASCO.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa akiwa anafuatilia namna Mtaalamu Usanifu Maabara wa Maji Ramadhan Zahoro wakati alipotembelea kisima kilichochimbwa katika Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa na Uhuru Mchanganyiko Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa akiangalia moja ya Kisima kilichochimbwa katika Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa na Uhuru Mchanganyiko Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kukagua kisima kilichopo Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa na Uhuru Mchanganyiko Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...