*Awataka wasikae ofisi wawe wabunifu
*awaambia DAWASCO wasiridhike na mapato waongeze idadi ya watumiaji maji.

WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa amezindua bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka (DAWASA) iliyo chini ya Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Julai 07 mwaka huu.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji amezindua bodi hiyo baada ya kukamilisha uteuzi wa wajumbe tisa wanaokamilisha Bodi ya DAWASA.Akizungumza wakati wa kuzindua bodi hiyo, Prof Mbarawa amesema kuwa ana imani na bodi iliyoteuliwa kuwa itafanya kazi kwa ufanisi mkubwa na kuleta maslahi mapana kwa wananchi .

Prof Mbarawa amesema anahitaji taasisi kama DAWASA kuwa wabunifu na kuweza kufanikisha upatikanaji wa wateja wapya ili huduma za maji ziwafikie watu wote pamoja na kuongeza pato la nchi.

Amesema kuwa, bodi hii wanaamini watasimamia vizuri utendaji wa kazi wa mamlaka hizi kwakuwa kumekuwa na upotevu mkubwa wa maji na hilo linasababishwa na baadhi ya viwanda kuiba maji na kuitia hasara serikali.

" katika viwanda vya bia asilimia 75 ya uzalishaji maji ndiyo yanatumika ila kumekuwa na upotevu mkubwa  sana wa maji na pia kuna kiwanda sitakiweka wazi ambao kwa mwezi wanatumia lita Milioni 60 za maji ambazo ni Milioni 2 kwa siku lakini ukija katika malipo yao wanasema wanatumia Lita Milioni 17,"amesema Prof Mbarawa.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange akizungumza baada ya bodi ya Wakurugenzi kuzinduliwa leo Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi  Jeneral Mstaafu Davis Mwamunyange, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Hapi na wajumbe wa bodi wakiwa katika picha ya pamoja.
 WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji, ProfesaMakame Mbarawa, akikabidhi vitendea kazi kwa mmoja wa wajumbe wa bodi ya DAWASA,katika uzinduzi wa bodihiyo, Dar es Salaam, leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, ProfesaMakame Mbarawa, akizungumza wageni waliofika wakati wa uzinduzi wa bodi ya wakurugenzi ya DAWASA pamoja na kuwapatia vitendea kazi kwa kila mmoja wa wajumbe wa bodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.

KWAPICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...