THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

RAIS MAGUFULI KUFUNGUA MKUTANO WA KIDUNIA WA VYAMA VYA KISIASA JIJINI DARNa Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kufungua Mkutano wa Kidunia wa Vyama vya Siasa (Mkutano maalum kwa Kanda ya Afrika) uliondaliwa na Chama cha Kikomonisti cha Watu wa China (CPC).
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema kuwa Mkutano huo utakao husisha Vyama 40 utakuwa wa kwanza kufanyika nje ya China na wa pili baada ya ule wa uliofanyika China.

Polepole amesema ni heshima kubwa kwa Serikali ya Tanzania, Nchi na Chama cha Mapinduzi (CCM) kutokana na Mkutano huo kuhusisha pia washiriki zaidi ya 200 kutoka Afrika na nje ya Afrika.

Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Uhusiano wa Afrika (IDCPC), Wang Heming amesema kuwa Mkutano huo unafanyika Tanzania ni kutoka ushirikiano mzuri ulikuwepo baina ya China na Tanzania, pia Tanzania ni nchi ambayo imehusika katika Ukombozi wa Bara la Afrika.

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika siku mbili ambapo utafunguliwa na Rais Magufuli, kesho Julai 17 na kufungwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi atakayemuwakilisha Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu mkutano wa kidunia wa vyama kiaiasa vya Barani Afika kwa ushirikiano na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC). Kushoto ni Mkurugenzi wa wa Mawasiliano kwa Umma, Sun Haiyan na kulia ni Naibu Mkurugenzi mkuu wa Uhusiano wa Afrika (IDCPC) Wang Heming.

Mkurugenzi wa wa Mawasiliano kwa Umma, Sun Haiyan(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu mkutano wa vyama vya siasa vipavyo 38 vilivyofika kuudhuria mkutano huo utakaofanyika kesho katika ukumbi wa hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.