MKUU wa mkoa wa Iringa Mh. Amina Masenza ametoa wito kwa wadau wa utalii na maendeleo nchini kuwekeza zaidi kwenye sekta ya Utalii katika Ukanda wa Nyanda za juu Kusini ili kuunga mkono adhma ya serikali ya kufungua na kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana katika kanda hiyo.

Bi. Masenza ametoa wito huo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Maonesho ya Utalii Karibu Kusini 2018 yanayoenda sambamba na Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani Kitaifa yanayotarajiwa kufanyika mkoani Iringa Septemba 26 hadi 30 mwaka huu.

Alisema kwa sasa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini imejipanga kimkakati kuhakikisha kwamba inatangaza na fursa na vivutio vya kiutalii vinavyopatikana katika mikoa hiyo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli alilolitoa hivi karibuni wakati wa kilele cha sherehe za Mei Mosi zilizofanyika kitaifa mkoani Iringa ambapo aliitaka mikoa hiyo kufunguka kiutalii.

Mikoa inayounda kanda hiyo ni pamoja na Iringa, Mbeya, Njombe, Songwe, Ruvuma, Rukwa na Katavi. 
“Mikoa ya nyanda za juu Kusini inasifika kuwa na hifadhi zenye sifa za kipekee ikiwemo Taifa ya Ruaha yenye makundi makubwa ya tembo na wanyama wengine. Hifadhi nyingine ni Kitulo yenye aina mbali mbali za maua ambayo hayapatikani mahali pengine Duniani; na Udzungwa yenye wanyama adimu duniani kama vyura wa Kihansi na mengine mengi,’’ alitaja. 

Akizungumzia maonesho hayo Bi Masenza alisema tofauti na miaka miwili iliyopita maonesho ya mwaka huu yataambatana na nyongeza ya matukio kadhaa ya kimichezo, kitaaluma na kiutamaduni ili kuongeza tija zaidi katika kufikia malengo ambayo hasa ni kuongeza mazao ya utalii katika kanda hiyo. 
MKUU wa mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Maonesho ya Utalii Karibu Kusini 2018 yanayotarajiwa kufanyika mkoani Iringa Septemba 26 hadi 30 mwaka huu. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Bw Richard Kasesela pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri Wilaya ya Iringa Bw. Robert Masunya. Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Bw Richard Kasesela (kushoto) akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkurugenzi Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Ernest Mwamwaja (kulia) akizungumza kwenye mkutano huo.
Mratibu wa Maonesho ya Utalii Karibu Kusini 2018 kutoka Kampuni ya Capital Plus Internantional (CPI) Bw Clement Mshana (katikati) akizungumza kwenye mkutano huo. Kampuni hiyo inashirikiana na Mkoa wa Iringa kuratibu maonesho hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...