NA WAMJW-MWANZA.
SERIKALI kupitia wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imefuta tozo ya usajili , kushikilia na kuhuwisha dawa zenye  wagonjwa nadra  kwa wawekezaji wote kupitia Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA).

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipotembelea kuangalia ujenzi wa jengo la TFDA ambalo linajengwa Jijini Mwanza ili kusogeza huduma kwa wananchi wa mkoa huo.

“Ili kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kukuza nchi kupitia uchumi wa viwanda hivyo TFDA msiwe kikwazo kwa wawekezaji hao hivyo kuanzia leo nafuta tozo za kusajili, kushikilia na kuhuwisha dawa (orphan medicines) ambazo zina idadi ndogo ya wagonjwa na magonjwa hayo ni hatarishi ili kuvutia wawekezaji katika eneo hili ”, alisema Waziri Ummy.

 Aidha, Waziri Ummy amewaagiza TFDA kuzipa kipaumbele dawa hizo wakati wa usajili.Aidha Waziri Ummy amesema kuwa kuendana na juhudi hizo pia Serikali  imefuta tozo ya udhibiti  ya thamani ya 0.25 za dawa,vifaa na vifaa tiba zinazoingizwa kwenye hospitali za Umma kutoka kwa wafadhili.
 Waziri wa afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katikati akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu Wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kushoto wakati alipotembelea kukagua shughuli za ujenzi wa jengo la Mamlaka hiyo jijini Mwanza. Kulia ni Mkurugenzi wa Ubora wa Huduma za Afya kutoka Wizara ya afya Dkt. Mohammed Mohammed.
 Waziri wa afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia akipata maelezo juu ya sukari zinazopimwa ubora wake  kutoka kwa Mkuu wa Maabara wa TFDA  Kanda ya Ziwa Bw. Salum Kindoli wakati alipotembelea kukagua shughuli za ujenzi wa jengo la Mamlaka hiyo jijini Mwanza.
 Waziri wa afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia  akipata baadhi ya maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Ubora wa Huduma za Afya kutoka Wizara ya afya Dkt. Mohammed Mohammed kushoto wakati alipotembelea kukagua shughuli za ujenzi wa jengo la Mamlaka hiyo jijini Mwanza.
 Waziri wa afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katikati akikagua shughuli za ujenzi wa jengo la wodi ya mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou toure wakati alipotembelea kukagua shughuli za ujenzi wa jengo hilo jijini Mwanza.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...