Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii,

Msemaji wa Idara ya Uhamiaji , Ally Mtanda ameainisha sifa za kuweza kupata hati ya kusafiria kwa njia ya kieletroniki.

Akizungumza na Michuzi Blog katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 42 ndani ya Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere  (Sabasaba).Mtanda amesema sifa za muombaji pasipoti lazima adhibitishe uraia wake pamoja na safari yake kuwasilisha  nyaraka za viambatanisho mbalimbali.

Amesema kuwa viambatanisho hivyo cheti/Kiapo cha kuzaliwa muomabji au cheti cha uraia ,Cheti cha kuzaliwa cha mmoja wa wazazi au ushahidi wa mmoja wa wazazi.


Mtanda amesema namna ya kujaza fomu katika mfumo wa kielektroniki ni kuingia katika tovuti ya idara hiyo ambayo ni www.immigration.go.tz.
 Msemaji wa Idara ya Uhamiaji , Ally Mtanda akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda la Idara ya Uhamiaji  Uhamiaji katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 42 katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere  (Sabasaba).
Mkaguzi Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji , Neema Mwakilembe akitoa maelezo namna ya kupata hati ya kusafiria kwa njia ya kielektroniki kwa wananchi waliotembelea banda la Uhamiaji katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 42 katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere  (Sabasaba).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...