Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inatarajia kuzindua huduma mpya ya kliniki ya moyo inayotembea (Cardiac Mobile Clinic) kwa kufuata wagonjwa popote pale walipo na kuwahudumia. Huduma hii maalum inatarajiwa kuzinduliwa mkoani Ruvuma tarehe 23/7/2018.

Kuanzishwa kwa huduma hii kutasaidia wananchi wengi hasa wa mikoani ambako ni mbali na Taasisi yetu ilipo kufikiwa kwa urahisi zaidi na kupata huduma za matibabu ya moyo ya kibingwa.

Baada ya kufanyika kwa uzinduzi huo tutaendelea kutoa huduma kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma kwa muda wa siku sita kuanzia tarehe 23-28/7/2018. Huduma hii ya kliniki inayotembea itakuwa endelevu katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani. Siku za karibuni tutatoa ratiba kamili kadri ya maombi yatakavyotufikia kutoka Tawala za Mikoa.

Huduma tutakazozitoa ni kutoa matibabu baada ya kufanya vipimo kwa kutumia mitambo mahususi tuliyokuwa nayo. Ushauri wa kiafya kuhusiana na Magonjwa ya Moyo, elimu ya lishe bora, kutoa Rufaa ya moja kwa moja kwa wagonjwa watakaokutwa na matatizo ya Moyo kuja kwenye Taasisi yetu kwa uchunguzi wa tiba zaidi.

Dhumuni la Taasisi ni kuhakikisha kila mgonjwa anapata huduma bora na kuwa na elimu inayohusiana na magonjwa ya Moyo. Wananchi wote wa mkoa wa Ruvuma pamoja na mikoa ya jirani tunawakaribisha mfike katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma (Songea) ili muweze kupata huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo.

Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...