Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

WAKALA wa mafunzo kwa Njia ya mtandao nchini (TaGLA) kwa kushirikiana na Wakala wa masuala ya teknolojia Afrika (ICDL) wamekutana na kujadili namna wanavyofanya kazi na changamoto wanazokutana nazo katika utendaji kazi sambamba na kuzitafutia suluhisho.

Akizungumza na vyombo vya habari Mkurugenzi Mtendaji wa ICDL Afrika Etinick Mutinda ameeleza kuwa nchi 17 ni mwananchama wa ICDL ambapo makao makuu yapo Kigali nchini Rwanda na bado wanashawishi nchi nyingine kujiunga kwa maendeleo zaidi.

Ameeleza kuwa lengo la ICDL ni kusaidia na kushirikiana na Serikali katika masuala ya kiteknolojia na namna ya kutumia teknolojia kwa manufaa ya kujenga taifa na wanashirikiana na Serikali pamoja na taasisi binafsi katika kuhakikisha teknolojia inasaidia katika kukuza uchumi na katika mkutano huo wataangalia changamoto na namna ya kuzikabili katika masuala ya tehama.

Akiiwakilisha wakala ya mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA) meneja habari na mafunzo Dickson Manyika ameeleza kuwa malengo ya teknolojia hasa matumizi ya kompyuta na mitandao yawe ya manufaa katika kushirikishana mawazo ambayo yataleta mabadiliko na maendeleo katika jamii.

Ameeleza kama wakala wana vipindi maalumu wanavyofanya kwa njia ya mtandao kwa kushirikiana na nchi mbalimbali na hujadili masuala ya kusaidia serikali na jamii kwa ujumla kama vile kukua na upangaji wa miji na masuala ya kielimu.

Baadhi ya washiriki wameeleza kuwa katika kuelekea uchumi wa viwanda hatuwezi kubaki nyuma katika suala la teknolojia kwani njanja nyingi kama kilimo, elimu na viwanda huhitaji matumizi ya teknolojia bora katika kufikia malengo.
 Meneja habari na mafunzo wa Wakala wa mafunzo kwa njia ya Mtandao,Dickson Manyika akizungumza na Globu ya jamii kuhusu matumizi ya mitandao iwe ya manufaa katika kushirikisha mambo mbalimbali ya maendeleo katika jamii.
 Mkurugenzi Mtendaji wa ICDL Afrika,Etinick Mutinda akizungumza na wadau mbalimbali wa mitandao katika mkutano uliofanyika leo jijini Dar as Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Semu ya wadau mbalimbali wa mitandao wakiwa katika mkutano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...