MKUU wa mkoa wa Kigoma Emmanuel Maganga amesema serikali ya Tanzania inafurahishwa na namna Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanavyofanya kila linalowezekana kusaidia kuboresha maisha ya wananchi wa mkoa wa Kigoma ambao ndio wenyeji wa wenzao wanaokimbia matatizo nchi jirani.
Akizungumza katika mkutano wa kamati ya maandalizi ya utekelezaji wa programu ya pamoja ya kusaidia Kigoma (KJP), alisema kazi kubwa inayofanywa na mashirika hayo ikiwamo ya kupeleka ushawishi kwa wadau wa maendeleo ya kusaidia wananchi wa Kigoma wakiwemo wageni wakazi na wakimbizi.
Akiwa Mwenyekiti mwenza wa kamati hiyo, Maganga alisema pamoja na juhudi hizo bado mkoa una changamoto nyingi zinazotakiwa kushughulikiwa japo serikali imeendelea na juhudi za kuboresha mazingira ya miundombinu ya kuwezesha shughuli za kiuchumi.
Alisema toka mkutano wa mwisho mwaka jana, kumekuwa na maendeleo makubwa katika kampeni za serikali za kuufungua mkoa huo kiuchumi kwa kutengeneza miundombinu mbalimbali kuifanya Kigoma kuwa kitovu cha biashara.
Alisema serikali inaendeleza miradi ya kimkakati hasa ya barabara zinazounga mkoa huo na nchi za Rwanda, Burundi, Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo (DRC) na mikoa mingine ya Tanzania ya Shinyanga, Mwanza, Kagera na Tabora.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitoa neno la ukaribisho
wakati wa mkutano wa kamati ya maandalizi ya utekelezaji wa programu ya
pamoja ya kusaidia Kigoma (KJP) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa
Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga na kulia ni
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo.
Mkuu
wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga (wa pili
kulia)akizungumza wakati akifungua mkutano wa kamati ya maandalizi ya
utekelezaji wa programu ya pamoja ya kusaidia Kigoma (KJP) uliofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es
Salaam. Wengine katika picha ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Charles
Pallangyo (kulia), Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa
pili kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini, Michael Dunford (kushoto).
Kansela
wa Ubalozi wa Norway, Britt Kjolas akitoa salamu kwa niaba ya wadau wa
maendeleo wakati wa mkutano wa kamati ya maandalizi ya utekelezaji wa
programu ya pamoja ya kusaidia Kigoma (KJP) uliofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo (kulia) akifafanua jambo
wakati wa mkutano wa kamati ya maandalizi ya utekelezaji wa programu ya
pamoja ya kusaidia Kigoma (KJP) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi
wa Umoja wa Mataifa Kigoma, Evance Siangicha akiwasilisha rasimu ya
makubaliano ya utekelezaji wa Programu ya KJP wakati wa mkutano wa
kamati ya maandalizi ya utekelezaji wa programu ya pamoja ya kusaidia
Kigoma (KJP) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa
Mataifa jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mchambuzi Mratibu wa Umoja
wa Mataifa (UN Coordination Analyst )nchini, Kanali Rankho
Mwakilishi
kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani (UNICEF)
nchini, Stephanie Shanler akiwasilisha hatua iliyofikiwa kwenye
utekelezaji wa mradi wa KJP eneo la kuzuia ukatili kwa wanawake na
watoto wakati wa mkutano wa kamati ya maandalizi ya utekelezaji wa
programu ya pamoja ya kusaidia Kigoma (KJP) uliofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) nchini, Viola Kuhaisa akiwasilisha hatua iliyofikiwa
katika utekelezaji wa eneo la elimu wakati wa mkutano wa kamati ya
maandalizi ya utekelezaji wa programu ya pamoja ya kusaidia Kigoma (KJP)
uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa
jijini Dar es Salaam.
Picha
ya pamoja ya washiriki wa mkutano wa kamati ya maandalizi ya
utekelezaji wa programu ya pamoja ya kusaidia Kigoma (KJP) wakiwemo
wadau wa maendeleo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za
Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...