KUMRADHI...
MABADILIKO KIDOGO YA RATIBA YA MUDA WA MAZISHI

Kwa niaba ya Familia ya Mama Salma Rashid-Kikwete na Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, nasikitika  kutoa taarifa kuwa jana Alhamisi Julai 19, 2018 Mama Salma Rashid Kikwete amefiwa na Baba yake Mzazi,  Mzee Rashid Mkwachu, katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Shughuli za Msiba  zitakuwa nyumbani kwa Mama na Dr. Jakaya Mrisho Kikwete Msasani jijini Dar es salaam. 

Mazishi yanatarajiwa kufanyika katika makaburi ya Kisutu  leo Ijumaa Julai 20, 2018 Saa tisa kabla ya Swala ya Alasiri (kunradhi, sio saa 10 kama ilivyotangazwa awali). Kisomo na dua vitafanyika hapo Msasani  kabla ya Swala ya Ijumaa.

Kwa niaba ya Familia 
Ridhiwani Kikwete


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...