Na Rachel Mkundai, Arusha

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imekuja na mkakati maalum wa kuhakikisha kwamba pato la Serikali na kodi stahiki inapatikana kupitia sekta ya utalii nchini.

Akizungumza Jijini Arusha, Kamishna wa Kodi za Ndani, Bwana ELIJAH MWANDUMBYAamesema kwamba, sekta ya utalii ni moja ya sekta inayoiingizia Serikali fedha nyingi za kigeni na hivyo inahitaji mkakati madhubuti ili kuongeza pato kwa Serikali

“Sekta ya utalii inaingizia serikali fedha nyingi za kigeni, TRA tumekuja na mkakati maalum ili kuhakikisha kuwa sekta hii inachangia pato la taifa kupitia kodi stahiki kwa mujibu wa sheria za kodi”, amesema Kamishna wa kodi za ndani.

Mwandumbya ameongeza kuwa kwa muda mrefu sekta ya utalii imekuwa ikifanya vizuri lakini bado inahitaji mkakati wa kuhakikisha kwamba kila pato linaloingia kupitia sekta hii linaongeza tija kwenye mapato ya nchi kupitia kodi mbalimbali kama zilivyoainishwa na sheria za kodi.

Aidha, Kamishna Mwandumbya amefafanua kuwa moja ya mikakati hiyo ni kushirikiana na taasisi zingine za serikali zilizopo kwenye sekta ya utalii zikiwemo Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Chama cha wafanyabiashara wa Utalii (TATO) pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii na wadau wengine wanaojihusisha na utalii.
Kamishna wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara ya Utalii (TATO), Bw. Wilberd Chambulo wakati wa ziara yake ya kikazi Jijini Arusha yenye lengo la kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta ya utalii nchini.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Arusha, Bw. Faustine Mdesa (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara ya Utalii (TATO), Bw. Wilberd Chambulo wakati wa ziara ya kikazi ya Kamishna wa Kodi za Ndani Jijini Arusha yenye lengo la kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta ya utalii nchini.
Kamishna wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya (kulia) akifanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara ya Utalii (TATO), Bw. Wilberd Chambulo wakati wa ziara yake ya kikazi Jijini Arusha yenye lengo la kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta ya utalii nchini.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara ya Utalii (TATO), Bw. Wilberd Chambulo (kushoto) akimwelezea jambo Kamishna wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya pamoja na watendaji wengine wa TRA aliofuatana nao kuhusu namna sekta ya utalii nchini inavyochangia pato kubwa kwa Serikali wakati wa ziara ya kikazi ya Kamishna huyo Jijini Arusha yenye lengo la kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta ya utalii nchini. (PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-TRA).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...