Na Rachel Mkundai

Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imetangaza msamaha wa riba na adhabu za madeni ya nyuma ya Kodi hadi asilimia mia moja ili kutoa unafuu kwa walipakodi wenye malimbikizo kulipa kodi ya msingi tu yaani “Principal Tax”

Akitangaza msamaha huo, Kamishna Mkuu wa TRA Charles Kichere amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa msamaha huo ni matokea ya utekelezaji  Maelekezo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa Baraza la Wafanyabiashara (TNBC) uliofanyika Ikulu tarehe 20/03/2018 ambapo wafanyabiashara walilalamikia kuwepo kwa malimbikizo makubwa ya madeni ya kodi za nyuma yakijumuisha riba na adhabu,

Kichere amesema kuwa, ili kukamilisha hilo, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limefanya marekebisho kupitia Sheria ya Fedha ya mwaka 2018 na sehemu ya Sheria ya Usimamizi wa Kodi ya Mwaka 2015. 

“Katika marekebisho hayo Waziri mwenye dhamana ya Fedha na Mipango amepewa mamlaka ya kutoa utaratibu maalum wa kuwezesha Kamishna Mkuu kutoa msamaha riba na adhabu wa hadi asmilia mia moja riba na adhabu kwenye malimbikizo ya madeni ya kodikwa asilimia mia moja tofauti na asilimia 50 ya hapo awali”, amesema.

Aidha, amebainisha kuwa lengo kuu la msamaha huu ni kutoa unafuu kwa walipakodi wenye malimbikizo ya madeni ya riba na adhabu kwa kuwapa fursa ya kulipa malimbikizo ya madeni ya msingi ya kodi “Principal Tax” kwa awamu ndani ya mwaka wa fedha 2018/19 ili kuwapa motisha ya kulipa kodi kwa hiyari na kwa Wakati.

Amesema kuwa msamaha wa riba na adhabu utahusu kodi zotezinazotozwa kwa mujibu wa Sheria zinazosimamiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania, isipokuwa: Ushuru wa Forodha unaosimamiwa chini ya Sheria ya Ushuru wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka 2004; na malipo  mengine yasiyo ya kodi ambayo TRA imepewa jukumu la kisheria la kuyakusanya. Mapato hayo ni kama vile: Kodi za Majengo na Ada za Matangazo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...