Mojawapo ya mbwembwe za mashabiki wapatao 7, 000 wa Uingereza waliomiminika jijini Moscow, wengine wakiwa wamevalia visibao kama kocha wao Gareth Southgate zimezimika  usiku huu ambapo badala ya kurudisha mwali nyumbani inabidi warudi labda na ushindi wa tatu. 
Croatia usiku huu imekuwa nchi 'tofauti' ya 13th kutinga fainali ya Kombe la Dunia la soka na ya 10 kutoka Ulaya kwa kuipiga Uingereza goli 2-1 katika dakika 120 baada ya kufungana 1-1 katika dakika 90 za kawaida. Shujaa wa Croatia yenye watu milioni 4 alikuwa ni huyo  Mario Mandzukic aliyetia kimiani bao katika dakika ya 11 kabla ya filimbi ya mwisho kwa pasi tamu ya kichwa toka kwa Ivan Perisic.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...