Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kukabiliana na vitendo vya uhalifu na ajali za barabarani ili kuhakikisha kuwa wageni na wakazi wa Mkoa huu wanaendelea kuwa salama na mali zao. Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kushirikiana na wananchi na wadau wengine wa usalama hali inayopelekea kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu pamoja na ajali za barabarani. 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea na Oparesheni ya kukagua magari pamoja na kukamata makosa mbalimbali ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani. Katika Oparesheni iliyofanyika mnamo tarehe 14.07.2018 kuanzia majira ya saa 05:00 alfajiri katika Stendi Kuu ya Mabasi jumla ya Mabasi 43 yaendayo Mikoa mbalimbali yamekaguliwa kati ya hayo 38 yaliruhusiwa kuendelea na safari wakati Mabasi 05 yaligundulika kuwa na hitilafu hivyo hayakuruhusiwa kuendelea na safari hadi yatakapo tengenezwa. 

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanya Oparesheni ya kushtukiza katika maeneo ya Kabwe, Mwanjelwa, Isanga, Soweto, Uyole na Iyunga na kufanikiwa kukamata magari 45 kati ya hayo 29 yamekutwa na makosa mbalimbali yakiwemo ya ubovu, kuvuja mafuta, kuisha kwa matairi na baadhi ya gari za abiria @ daladala kuchakaa kwa viti vya kukalia abiria.

Kufuatia Oparesheni hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ULRICH MATEI amewataka madereva kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kuepuka ajali za mara kwa mara. 

Aidha Kamanda MATEI amewataka wamiliki wa vyombo vya moto hasa magari kujenga utaratibu wa kuyafanyia matengenezo ya mara kwa mara magari yao ili yaweze kutumika kikamilifu katika kazi ya kubeba na kusafirisha abiria vinginevyo Jeshi la Polisi litawachukulia hatua za kisheria wamiliki wote ambao magari yao yatabainika kuwa mabovu hali inayoweza kupelekea ajali.

Imesainiwa na: 
[ULRICH O. MATEI - SACP] 
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...