Ni utalii katika msitu wa Chome hususan kilele cha mlima Shengena ambapo Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro imedhamiria kutangaza kivutio hiki ili kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea eneo hilo. 
Mkuu wa Wilaya ya  Same Mhe. Rosemary Sitaki aliongoza wataalamu 23 toka ofisi za serikali Wilayani hapo wakiratibiwa na Wakala wa Misitu (TFS)  kupanda mlima Shengena wenye urefu wa Mita 2462 toka usawa wa bahari, ambacho ni kilele cha pili kwa urefu kufuatia Mlima Kilimanjaro.
Mlima huo una vivutio  vingi vya miti, ndege, vipepeo,  nyani, mito na uoto wa asili ni raslimali kubwa. 
Ni eneo unaloona Mlima kilimanjaro kwa juu zaidi kuliko eneo jingine lolote, na linafaa kwa utalii, mazoezi ya kupanda mlima Kilimanjaro, kurekodi Sinema, hifadhi ya mazingira, uwekezaji, utafiti, vyanzo vya maji, camp site ambapo 
TFS wanafikiria kuweka "sky line"
" Ni lazima tujipange kufanya vitu tofauti ili kuwafanya watalii kuchagua Shengena" alisema DC Sitaki, huku akiwaalika wananchi na wageni  kuja kujionea uumbaji wa ajabu wa Mungu uliopo Shengena. 
Alitoa tahadhari kwa wenye nia ya kuchezea msitu huo, kwa kuwa ni moyo ya Wilaya ya Same kwani vyanzo vya maji zaidi ya 8 vinavyotegemewa na Wananchi vinaanzia msitu huo. Aliahidi kuutunza, kuulinda  kuuthamini na kuwachukulia hatua wanaouchezea. 
Timu hiyo ilitumia kati ya saa 2.30 - 2.40 kufika kileleni umbali wa Km. 5.54. 

 Mkuu wa Wilaya ya  Same Mhe. Rosemary Sitaki (kilemba cha buluu) na  wataalamu 23 toka ofisi za serikali Wilayani hapo wakipumzika baada ya  kupanda mlima Shengena wenye urefu wa mita 2462 kutoka usawa wa bahari.
 Mkuu wa Wilaya ya  Same Mhe. Rosemary Sitaki (kilemba cha buluu) akiongoza   wataalamu 23 toka ofisi za serikali Wilayani hapo wakipumzika baada ya  kupanda mlima Shengena wenye urefu wa mita 2462 kutoka usawa wa bahari.
 Mkuu wa Wilaya ya  Same Mhe. Rosemary Sitaki (kilemba cha buluu) na  wataalamu 23 toka ofisi za serikali Wilayani hapo wakiwa kwenye kilele cha  mlima Shengena wenye urefu wa mita 2462 kutoka usawa wa bahari.
Mtaalamu akitoa maelezo juu ya kilele cha mlima Shengena

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...