Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii
NAOMBA kutumia nafasi hii kwanza kabisa kutoa salamu kwa Watanzania wote. Pili naomba nitoe salamu zangu za unyenyekevu kwa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano Dk. John Magufuli.
Baada ya salamu hizo pia naomba nitumie nafasi hii kupongeza jitihada za Rais Magufuli katika kuwatumikia Watanzania wote na kubwa zaidi harakati zake za kuhakikisha tunapiga hatua.
Pia, ahsante Rais Magufuli kwa jitihada zako ambazo umekuwa ukizifanya katika kuhakikisha tunakuwa nchi ya kujitegemea kupitia rasilimali ambazo Mwenyezi Mungu ametujaalia katika nchi yetu.
Ila Rais nikunong'oneze kuwa ujio wa Dreamliner umenikosha sana kama si kunifurahisha. Ni juzi tu macho ya Watanzania yameshuhudia ujio wa ndege hiyo kubwa na ya kisasa.Inahitaji uwe na akili za wendawazimu ili uweze kukosoa ujio wa ndege hiyo. Pia, inahitaji kujitoa ufahamu ili upate nafasi ya kuupotosha umma kuwa ujio wa Dreamliner haustahili.
Kwa mwenye akili timamu na anayejua nini maana ya maendeleo ataungana  na watanzania wote kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa uamuzi wa kununua ndege kwa lengo la kuliboresha Shirika la Ndege la ATCL. Ahsante Rais.Baada ya utangulizi huo nielezee hivi leo hii nimeamua kujikita katika kuzungumzia urafiki kati ya nchi za Tanzania na China. 
Nazungumzia urafiki huo nikitambua kuwa Julai 17 mpaka Julai 18 mwaka huu Tanzania inapokea ugeni mkubwa ambao utahudhuria mkutano wa kidunia ambao unahusisha vyama vya kisiasa ambavyo vilikuwa mstari wa mbele kupigania ukombozi kwa nchi za Kusini mwa Bara la Afrika.

Mkutano huo utafanyika jijini Dar es Saalam. Ni mkutano ambao umeandaliwa na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC). Ni mkutano  mkubwa haswaa. Yaani mkubwa naomba unielewe. Kwa msisitizo niandike kwa herufi kubwa kwamba NI MKUTANO MKUBWA SANA.
Hivyo kabla ya kuzungumzia mkutano huo niombe nizungumzie alau kwa uchache urafiki wa miaka mingi kati ya Tanzania na China. Kwa kukumbusha tu uhusiano kati ya Tanzania na China umeleta faida kubwa za kimaendeleo.Kupitia urafiki huo kuna mambo mengi Watanzania tumenufaika nayo na wao China yapo mambo mengi ambayo wamenufaika nayo kutoka na urafiki wao na sisi.Uhusiano wa China na Tanzania umekuwa na mafanikio makubwa ya kuziunganisha nchi hizo katika kusaidiana katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo.
Kila mmoja anaweza kuelezea namna anavyoona inafaa kuhusu uhusiano kati ya nchi hizo mbili lakini jambo la msingi na la kuzingatiwa Tanzania na China wamekuwa na urafiki wa muda mrefu uliofanikisha mambo mengi kufanyika.Kumbukumbu zinaonesha baada tu ya uhuru wa Tanganyika na Zanzibar, wataalam wa kilimo, ujenzi na madini walifika kusaidia wenzao wa Tanzania katika fani zao.
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mhe Guo Jinlong na ujumbe wake  walipowasili Ikulu jijini Dar es salaam Machi 22, 2017 
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongozana na Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mhe Guo Jinlong  walipowasili Ikulu jijini Dar es salaam Machi 22, 2017.
PICHA NA IKULU.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...