Na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii 

BARAZA kuu la Umoja wa Vijana kupitia Chama Cha CCM(UVCCM)Wilaya ya Mkuranga limefanya kikao kwa lengo la kutatua changamoto zinazowakabili vijana.

Akizungumza na wanahabari Mwenyekiti wa Baraza Kuu la umoja wa vijana Wilaya ya Mkuranga Mbwera amesema vijana wanachangamoto nyingi lakini CCM kina mikakati mbalimbali ya kuzitatua. 

Amefafanua tayariasa Mbunge wao amewatafutia fursa ya kutoa mikopo kwa ajili ya vijana .Pia amesema Mwenyekiti wa wauza ya pikipiki nchini tayari amezungumza na vijana kujitokeza kukopeshwa kuanzia bodaboda 50 ikiwa ni fursa ambayo imetafutwa na Mbunge wa jimbo la Mkuranga na kuhaidi kuwa vijana hawatomuangusha na marejesho yatarejeshwa kwa wakati.

Amefafanua kwa vijana ambao hawakufika katika mkutano huo wafahamu kuwa maendeleo yataletwa na CCM. Hivyo wajitokeze kwenye mikutano hiyo kwani ndio fursa peke yakujua matatizo ya jimbo hilo .Kwa upande wa Mjumbe wa Baraza Kuu la umoja huo Taifa Mkoa Ramadhani Mwishehe amewaomba wana CCM na wananchi kwa ujumla kuunga mkono juhudi za Rais Dk. John Magufuli za kuleta maendeleo.

Mwishehe amesema kuwa "vijana kimsingi tuige na kumuunga mkono kwani dhamira yake ni njema katika kutukomboa na kuleta maendeleo katika nchi yetu kwani kwa hali ya sasa ni tofauti na hapo wali."Ameongeza kuwa Sera ya kwanza ambayo alihimiza Rais pindi atakapoingia madarakani ni pamoja na elimu bure ambayo sasa itatolewa bure.

Mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa mkoa wa Pwani,Ramadhani Mlao akizungumza na vijana mara baada ya kufungua kutano wa Baraza kuu uliofanyika wilaya Mkuranga mkoa wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii.

Mwenyekiti wa Baradha kuu la umoja wa UVCCM wilaya Mkuranga,Ally Mohammed Mbwera akifafanua juu ya mikakati ya chama hicha kwa upende wavija Katika mkutano uliofanyika wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.
 Mkutano wa Baraza kuu la umoja wa UVCCM wilaya Mkuranga ukiendelea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...