THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

VIGOGO WATANO WA KNCU LTD,TCCCO WAFIKISHWA MAHAKAMANI LEO KWA MASHTAKA YA UHUJUMU UCHUMI

Na Dixon Busagaga,Moshi

VIONGOZI watano wa Chama cha Ushirika mkoa wa Kilimanjaro(KNCU LTD) na Kiwanda cha Kukoboa Kahawa cha Tanganyika (TCCCO) leo wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ,Moshi na kusomewa Mashtaka tofauti yakiwemo ya uhujumu Uchumi.

Waliofikishwa Mahakamani na kupandishwa Kizimbani ni pamoja na Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Kikuu cha Ushirika ,Kilimanjaro (KNCU) Aloisi Kitau (70) Makamu Mwenyekiti mstaafu wa KNCU,Hatibu Mwanga(70) na Meneeja Mkuu wa KNCU ,Honest Temba (38).

Wengine waliofikishwa mahamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi ,Pamela Mazengo ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Kukoboa Kahawa (TCCC0) Maynard Swai (57) na aliyekuwa Meneja Mkuu wa TCCCo ,Andrew Kleruu wanaotajwa kukiuka sheria wakati wa ununuzi wa mtambo wa kukoboa Kahawa.

Wakili wa serikali Jaqueline Nyantori aliieleza mahakamani kuwa Washitakiwa ,Maynard Swai na Andrew Kleruu wanakabiliwa na makosa mawili huku akiyataja kuwa ni Matumizi mabaya ya ofisi na kusababishia serikali hasara .

Upande wa Jamhuri katika Shauri hilo unawakilishwa na Wakili wa serikali Mandamizi ,Shadrack Martin,Wakili wa serikali Mwandamizi ,Abdalah Chavula na Wakili wa serijali Jacqueline Nyantori huku Wakili Julius Semali akimtetea Mshtakiwa Honest Temba na Wakili Captain Sawayaeli Shoo akimtetea Mshtakiwa Hatibu Mwanga.Watuhumiwa hao wakishushwa Mahakamani mapema leo chini ya Ulinzi wa Jeshi la Polisi,kusomewa mashtaka yao