Na Mwandishi wetu
WABUNGE wa mkoa wa Kigoma walipata nafasi ya kutaarifiwa mradi wa pamoja mkoa wa Kigoma na Umoja wa Mataifa ambao umejikita katika kutekeleza Mpango wa Taifa wa Maendeleo na pia kutekeleza shughuli mbali mbali zinazolenga kufikia malengo endelevu ya dunia.
Akifungua mkutano huo Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga aliwataka washiriki wa mkutano huo kufuatilia kwa makini hatua iliyofikiwa ya mradi huo na kutoa mapendekezo yao.
Baadhi ya shughuli za mradi huo zimeanza kutekelezwa hususan katika maeneo ya Kilimo, uwezeshaji wa wanawake na vijana kiuchumi, kutokomeza vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto na kina mama pamoja na elimu.
Mkuu huyo wa mkoa aliwataka waheshimiwa wabunge kutumia fursa waliyoipata kupokea taarifa kuhusu mradi na kutoa ushauri wa namna ya kufanikisha malengo yaliyowekwa ili kuwaletea maendeleo kwa wananchi wa mkoa wa Kigoma.
“Mkoa wa Kigoma ni Mkubwa na tunatamani kuona mradi huu unapanuka kujumuisha wilaya zote na pia sekta nyingine muhimu kama afya. “ alisema Maganga ambaye alisema kama serikali wako tayari kushirikiana na wadau wote wenye mapenzi na mkoa wa Kigoma wataliona hilo.
Katika mkutano huo ambao pia umehudhuriwa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez na wadau wengine wa maendeleo, misingi imara ya ushirikiano kwa ufanikishaji wa maendeleo ya mkoa wa Kigoma kwa ujumla yalizungumzwa na kuafikiwa.
Mkuu
wa mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga (kulia)
akifungua mkutano ulioandaliwa kwa Wabunge wa mkoa wa Kigoma juu ya
mradi wa pamoja na Umoja wa Mataifa uliofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam. Katikati ni
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na kushoto ni Katibu Tawala
wa Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitoa neno la ukaribisho
kutoka Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano ulioandaliwa kwa Wabunge wa
mkoa wa Kigoma juu ya mradi wa pamoja mkoa wa Kigoma na Umoja wa Mataifa
(UN-KJP) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa
Mataifa jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa
Kigoma, Charles Pallangyo na kushoto ni Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa
Kigoma, Evance Siangicha.
Mwenyekiti
wa Wabunge wa mkoa wa Kigoma ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kasulu
Mjini-CCM, Daniel Nsanzugwanko akitoa salamu kwa niaba ya Wabunge wa
mkoa wa Kigoma wakati mkutano ulioandaliwa kwa Wabunge hao juu ya mradi
wa pamoja na Umoja wa Mataifa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi
wa Umoja wa Mataifa Kigoma, Evance Siangicha (kulia) akiwasilisha
muhtasari wa mradi wa pamoja wa Umoja wa Mataifa kwa Wabunge wa mkoa wa
Kigoma wakati wa mkutano maalum ulioandaliwa juu ya mradi huo wa pamoja
uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa.
Mbunge
wa Kigoma Kaskazini kupitia tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe
akifafanua jambo wakati wa majadiliano juu ya mradi wa pamoja wa Kigoma
na Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano maalum na Wabunge wa mkoa huo
ulioandaliwa na UN na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za
Umoja wa Mataifa.
Kaimu
Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Faith Shayo (kulia) akielezea
kuhusu mradi wa UNESCO kwa kushirikiana na UN Women pamoja na UNFPA
unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Korea (KOICA) katika eneo la
elimu wakati wa mkutano juu ya mradi wa pamoja wa Kigoma na Umoja wa
Mataifa wakati wa mkutano maalum na Wabunge wa mkoa huo ulioandaliwa na
UN na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa.
Picha
ya pamoja ya Waheshimiwa Wabunge wa mkoa wa Kigoma na Wafanyakazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa mara baada ya kumalizika kwa mkutano
maalum juu ya mradi wa pamoja wa Kigoma na Umoja wa Mataifa na Wabunge
hao ulioandaliwa na UN na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi
za Umoja wa Mataifa.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...