THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

WAHASIBU WATATU WA TTCL KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA WIZI WAKIWA WATUMISHI

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Wahasibu watatu wa shirika la Mawasiliano Tanzania, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za wizi wakiwa watumishi na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya sh milioni 57.

Akisoma hati ya mashtaka, wakili wa serikali Mwandamizi, Patrick Mwita, amewataja washtakiwa hao kuwa ni, Mercy Semwenda (49)  Flora Bwahawa (54) na Hawa Tabuyanja(54).

Mbele Hakimu Mkazi, Augustine  Rwizile imedaiwa, mshtakiwa Semwenda  peke yake anadaiwa, kati ya Januari Mosi mwaka 2017 na Septemba 21 mwaka 2017 jijini Dar es Salaam,  aliiba vocha za muda wa maongezi za TTCl zenye thamani ya sh 44,393,000/ pamoja na fedha za mauzo ya Vocha zenye thamani ya sh milioni 5,914000/

Imedaiwa kuwa, mshtakiwa alifanya uwizi huo kutokana na kamba alikuwa mfanyakazi wa TTCL kama Mhasibu. Katika shtaka la pili imedaiwa, siku na mahali hapo, washtakiwa wote, waliisababishia Shirika la Mawasiliano  Tanzania, (TTCL), hasara ya sh. Milioni 57,773,122.

Hata hivyo, washtakiwa hao hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakamani hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi hadi Mahakamani kuu au kwa kupata kibali kutoka kwa DPP

Kufuatia hivyo, kesi imeahirishwa hadi Julai 24.2018 kwa ajili ya kuja kutajwa, kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika, watuhumiwa wote wamerudishwa rumande.
 Wakili anayewatetea washtakiwa hao amedai, ingawa mashtaka dhidi ya washtakiwa hao yanadhamana lakini wameshtakiwa kwa sheria ya uhujumu uchumi, basi atafuata taratibu zote za kisheria kuomba dhaman Mahakama kuu.