Na Mwandishi Maalum - DAKAWA
Wakulima wa kilimo cha Mpunga katika skimu ya kilimo cha Umwagiliji ya Dakawa wamenufaika na kilimo hicho baada ya serikali kukarabati mindombinu ya umwagilijai ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara, ofisi, ukarabati wa pump na  mifereji ya upili.
Hayo yameelezwa Mjini Dakawa na  Mhandisi wa Kanda ya Morogoro kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Senzie Meeda, alipozungumza na waandishi wa habari  walipotembelea skimu ya umwagiliaji ya Dakawa.
Mhandisi Meeda, ameeleza kuwa Serikali kupitia shirika la kimaitaifa la misaada la Marekani USAID lmetumia takribani kiasi cha shilingi Bilioni 20, katika ujenzi wa skimu hiyo,  na mpaka sasa asilimia themanini (80%) ya kazi hiyo inaendelea vizuri na inategemea kukamilika mwezi December mwaka huu.
“Njia zote za kwenda mashambani zinapitika, maeneo ya pembezoni ambayo yalikuwa hayafikiki mwanzoni sasa yanafikika, Pump Mpya za kisasa zinazotumia umeme mdogo zimefungwa hivyo uzalishaji umeongezeka ambapo mkulima anaweza kuvuna hadi tani sita (6) kwa hekta hili limesaidia sana kuongeza kipato na kutengeneza ajira.” Alisema Mhandisi Meeda.
Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa chama cha wakulima wadogo wa umwagiliaji Dakawa Bi.  Bertha Chilosa, ametoa shukrani kwa serikali kwa niaba ya wakulima wa dakawa na kusema kuwa kilimo kimekuwa na uchumi mkubwa katika eneo hilo na kubadilisha maisha yao na kuiomba serikali kuwasaidia wakulima hao kutafuta masoko ya uhakika ili kuwe na bei ya uhakika.
“Naiomba serikali itusaidie katika jambo hili, maana kutokuwa na soko la uhakika kunasababisha madalali wanakuja hapa kununua mpunga kwa bei ya kulangua na kutasababishia sisi wakulima wadogo kupata hasara, Naiomba serikali ichukue jukumu hili, ili mkulima asinyanyasike, sambamba na hili, ninaiomba serikali iongee na Mabenki ili yaweze kutupunguzia riba katika mikopo tunayopewa.” Alisisitiza Bi. Bertha
Skimu ya kilimo cha umwagiliaji ya dakawa ambayo ipo chini ya mradi wa Irrigation and Rural  Roads, katika program ya Feed the Future ina ukubwa wa hekta 3225 ambapo hekta 2000 zina miundombinu ya umwagiliaji, hekta 1000 bado hazijaendelezwa na hekta 225 ni za makazi na huduma za kijamii.
Shamba hilo la Dakawa lilijengwa na kumilikiwa na serikali kwa kupitia NAFCO tangu mwaka 1981 hadi mwaka 2003, na mwaka 2008 katika kubinafsisha mashirika ya umma  likakabidhiwa kwa ushirika wa wakulima wadogo Dakawa.
Na imeelezwa chama cha wakulima wadogo wa kilimo cha umwagiliaji dakawa, kina jumla ya wanachama 850 ambapo 500 ni wanaume na 350 ni wanawake.
  Mhandisi wa kanda ya Morogoro, kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Senzie Maeda, akiongea na waandishi wa habari katika skimu ya kilimo cha Umwagiliaji cha Dakawa, kilichopo katika Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro.
 Miundombinu inayopeleka maji katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji cha Dakawa iliyojengwa na Shirika la Kimataifa la misaada la Marekani (USAID) kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliji.

 Mwenyekiti Msaidizi wa cha Chama cha wakulima wa umwagiliaji Dakawa Bi.Bertha Chilosa akiongelea  Mafanikio na baadhi ya changamoto zinazowakabili wakulima katika kilimo hicho.
 Moja ya shamba la mpunga lililopo katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji cha Dakawa mkoani, Morogoro.


Wakulima wakiweka katika magunia  mpunga uliyovunwa na kifaa maalum cha kuvunia zao hilo katika moja ya shamba lililopo katika skimu ya umwagiliaji ya Dakawa mkoani Morogoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...