Wakulima katika eneo la Dakawa Wilayani Mvomero, wameiomba Serikali kuwaongezea eneo ambalo halitumiki kwa shughuli yoyote ile waweze kulitumia kwa kilimo cha mpunga.

Maombi hayo yametolewa baada ya kukamilika kwa ukarabati wa eneo lenye ukubwa wa hekta (2000), ambapo wananchi wamepata hamasa ya kulima baada ya kuona mafaniko ya tokanayo na kilimo cha umwagiliaji.

Akizunguma na waandishi wa habari katika skimu ya Dakawa, Mhandisi wa kanda ya Mororgoro kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Senzia Maeda, amesema Serikali kupitia Tume hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Misaada la Marekani USAID pamoja na kampuni ya SDM Smith ambayo imesanifu ukarabati wa eneo la awali imeshafanya upembuzi yakinifu kwa Hekta (500) katika hizo hekta (1000) na amesema kuwa makablasha ya zabuni yapo tayari.

“Hatua inayoendelea kwa sasa ni kwa Serikali kuu kupitia Tume kutafuta mfadhili kwa ajili ya kuendeleza hilo eneo.” Alisisitiza Maeda. Na aliongeza kwa kusema kuwa Serikali ilifikia uamuzi wa kuendeleza eneo la Dakawa baada ya kuridhishwa na ukulima wa kisasa

Awali, Akiongea na waandishi wa habari Ofisini kwake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mvomero, Bw. Florent Kyombo amesema pamoja na eneo hilo kuwa katika hatua nzuri ya uendelezwaji, Idara ya kilimo kupitia serikali ya wilaya na wataalam wa kilimo imeweza kuthibiti panya waharibifu wa mazao pamoja na ndege aina ya kwelea kwelea kwa kuharibu mazalio yao yote pamoja na suala zima la kuwasadia wakulima kupata mikopo katika baadhi ya mabenki nchini.

Bw. Arcado Ruhengiza ni mmoja wa wakilima katika skimu ya Dakawa ambapo yeye alisema kuwa endapo serikali itaongeza eneo kwa ajili ya kilimo cha mpunga, itawawezesha wakulima wengi zaidi kulima kisasa na kukuza sekta ya kilimo nchini kutokana na mafanikio waliyoyapata kupitia shamba hilo.

Mhandisi wa kanda ya Mororgoro kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Senzia Maeda, akiongea kuhusu upanuzi wa eneo lenye ukubwa wa Hekta (1000) kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji katika skimu ya Dakawa, wilayani Mvomero.
Ghala la kuhifadhia mazao lililojengwa na serikali katika skimu ya Dakawa wilayani Mvomero, ili kuweza kuwasaidia wakulima kuuza mazao yako kwa bei nzuri.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Bw. Florent Kyombo akiongea na waandishi wa Habari Ofisini kwake kuhusu mpango mzuri wa Serikali kwa wakulima wa kilimo cha mpunga kinachofanyika katika skimu ya Dakawa.
Katika Picha, Mkulima Bw. Arcado Ruhengisa akitoa Ombi la Upanuzi wa eneo lenye ukubwa wa Hekta (1000) kwa Serikali kupitia baadhi ya vyombo vya habari, ili wakulima waweze kongeza pato la Taifa, ajira kwa vijana na chakula kupitia kilimo cha umwagiliaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...