NA TIGANYA VINCENT

POLISI Mkoa wa Tabora linawashikiria watu 18 kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kuwachoma moto na wengine kushiriki katika mauaji. Kauli hiyo ilitolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Emmanuel Jackson. Alisema watuhumiwa 16 wanashikiriwa kwa tuhuma cha kujaribu kuwaua wanawake wanne kwa kuwachoma moto.

Kamanda huyo alisema wananchi kwa kushirikiana na Polisi wa wilaya ya Kaliua waliweza kuwaokoa wanawake hao wanne waliokuwa wamekamatwa na walinzi wa jadi zaidi ya miambili.

Kamanda Jackson alisema kuwa julai 16 mwaka huu saa nne usiku huko msitu wa Hifadhi ya Isawima kata ya Igwisi wilaya ya Kaliua kiongozi wa Sungusungu aitwaye Ingese Irea akiwaongoza wenzake 200 na kuwakamata akinamama wanne.

Alisema kuwa watu hao waliwakamata akinamama hao waliotambuliwa kwa majina ya Velediana Paulo (70), Modesta Magazi (45), Joyce Elias Magazi (33) na Nyamizi Dotto (40) walitaka kuwaua wakiwatuhumu kuwa ni wachawi.

Kamanda huyo aliongeza kuwa watuhumiwa hao na wenzao ambao bado wanasakwa baada ya kuwakata wakina mama hao walikusanya kuni nyingi na kisha kuwasha moto kwa dhumuni la kuwachoma.

Jackson alisema kuwa wakati watuhumiwa wakiendelea na za kufanikisha unyama huo taarifa toka kwa wananchi wema zilifika Polisi ambao bila kukawia walifika eneo la tukio na kuwaokoa na kufanikiwa kuwakamata baadhi yao.

Matukio ya aina hii ambayo yameegemea kwenye imani za kishirikina yanaendelea kushamiri katika vijiji mbali mbali vya mkoa wa Tabora hasa ambako wanaishi jamii ya wafugaji wa kabila la Wasukuma na kuupa mkoa sifa mbaya.

Mwishoni mwa mwaka uliopita watu wengine 55 wakazi wa kata ya Loya wilaya ya Uyui mkoani hapa akiwemo mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho walikamatwa baada ya jaribio lao la kutaka kuwaua wakina mama wanne kwa kuwachoma moto kwa imani hizo hizo kushirikana.

Wakati huo huo jeshi la Polisi linamshikiria Maganga Machibya (22) anayetuhumiwa kumuua Edina Mayunga mkazi wa kijiji cha Ifumba Wilaya ya Nzega kwa kumkata shingo kutokana na imani za kishirikina.

Katika tukio jingine la mauaji Abdalah Salehe mkazi wa Ipuli Manispaa ya Tabora anashikiliwa kwa tuhuma za kumuua mkewe Regina Athuman kwakumpiga na kisha kumnyonga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...