Na Dixon Busagaga,Same.

UBALOZI wa Kuwait nchini Tanzania umetoa jumla ya tani saba za msaada wa Chakula kwa waathirika wa Mafuriko wilayani Same mkoani Kilimanjaro ambao walilazimika kuyahama makazi yao katika Vijiji vya Kajiungeni na Ruvu Marwa na kuhamishiwa katika Makambi.

Msaada huo uliowasilishwa na Baloziw wa Kuwait nchini ,Jaseen Al Najem umetokana na jitihada za Waziri wa Madini ,Angela Kairuki za kusaidia kaya zilizofikwa na athari ya mafuriko hayo ambapo yeye binafsi alitoa Blanketi 300 na Turubai 200 kwa ajili ya wathirika hao kujisitiri.

Akizungumza wakati wa kukabidhi Msaada huo ,Balozi wa Kuwait ,Al Najeem amesema mbali na msaada huo anatarajia kuzungumza na Shirika la Huduma ya kwanza la nchini Kuwait kuona namna ambavyo watashirikiana na Shiriki la Msalaba mwekundu kusaidia wananchi hao.

Akitoa taarifa ya athari ya Mafuriko hayo Mkuu wa wilaya ya Same ,Rosemery Senyamule amesema wananchi wamekubalina kuhama kutoka eneo la Mafuriko ambalo wamekuwa wakifanya shughuli za Kilimo na kupewa maeneo ambayo sasa watafanya makazi ya kudumu.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania ,Jaseen Al Najem akikabidhi msaada wa Chakula kwa wananchi wa eneo la Kombo wilayani Same.kushoto ni Waziri wa Madini,Angela Kairuki na Mkuu wa wilaya ya Same,Rosemery Senyamule.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza Waziri wa Madini ,Angela Kairuki aliyeongozana na Balozi wa Kuwait nchini ,Jaseen Al Najem kutoa msaada kwa Wahanga hao.


Waziri wa Madini,Angela Kairuki akikabidhi msaada wa Blanketi na Maturubai kwa ajili ya kujengengea mahema ya muda kwa wahanga wa Mafuriko katika wilaya ya Same.
Waziri wa Madini,Angela Kairuki akisalimiana na mmoja wa Wazee ambao kwa sasa wanahifadhiwa na Majirani baada ya nyumba yake kuzingirwa na Mafuriko .

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...