Na Hamza Temba-Simiyu
*Atoa miezi mitatu kwa Muwekezaji kurudisha Serikalini hati miliki ya kipande cha ardhi kilichopo ndani ya Pori hilo

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amewapa siku 45 wananchi wanaoishi kinyume cha Sheria ndani ya kinga (buffer zone) za Pori la Akiba Kijereshi kuondoka kwa hiari yao wenyewe kabla ya kuanza operesheni ya kuwaondoa kwa nguvu.
 
Ametoa agizo hilo jana alipotembelea pori hilo katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu ikiwa ni muendelezo wa ziara zake mikoani kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi na kutatua changamoto zake.

Baada ya kushuhudia makazi na shughuli nyingine za kibinadam ndani ya pori hilo, Dk. Kigwangalla aliamua kutoa agizo hilo na kusema kuwa sheria za uhifadhi wa wanyamapori haziruhusu vitendo hivyo ndani ya maeneo yaliyohifadhiwa kisheria pamoja na kingo zake (buffer zone) ambazo ni mita 500 kutoka kwenye mpaka halisi wa eneo la hifadhi.

"Mpaka itakapofika tarehe 31 mwezi ujao (Septemba) wananchi wote hawa wawe wameshaondoka eneo hili kwa hiari yao wenyewe, muwatangazie na mpime eneo hili vizuri muweke alama ili wajue ni wapi wanatakiwa kuondoka.

"Na ikifika tarehe 1 Septemba kama kuna watakaokuwa wamekaidi agizo hili, basi mfanye oparesheni maalum muwaondoe na msafishe kila kitu, ni lazima ifike mahali kila mmoja aheshimu sheria za nchi" alisema Dk. Kigwangalla kuuagiza uongozi wa pori hilo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa mipaka ya Pori la Akiba Kijereshi na Meneja wa pori hilo, Dianna Chambi alipotembelea pori hilo jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu. Alitoa siku 45 kwa wananchi wote waliovamia kingo/bafa za hifadhi hiyo kuondoka kwa hiari yao. Kulia ni Mkuu wa Kanda wa Kikosi Dhidi ya Ujangili (KDU) Kanda ya Serengeti, Johnson Msella.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maelekezo kwa Meneja wa Pori la Akiba Kijereshi, Dianna Chambi (wa pili) kuhusu wananchi waliovamia hifadhi hiyo alipotembelea pori hilo jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akifungua koki ya maji katika eneo la hoteli ya kitalii ya Kijereshi Tented Camp iliyopo ndani ya Pori la Akiba Kijereshi alipotembelea pori hilo jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu, ametoa miezi mitatu kwa mmiliki wa hoteli hiyo kurudisha hati miliki ya kiwanja chenye hekta 464 kilichopo ndani ya pori hilo kwa kamishna wa ardhi kwakuwa ni batili na aendelee kutoa huduma kwa kuzingatia sheria na taraibu za uwekezaji.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua moja ya eneo la kingo/bafa la Pori la Akiba Maswa ambalo limevamiwa na wananchi kwa ajili ya shughuli kilimo alipolitembelea pori hilo jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu. Kulia kwake ni Mbunge wa Itilima, Njaru Silanga na Meneja wa Pori hilo, Lusajo Masin.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...