Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii,Globu ya Jamii
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Joyce Ndalichako, amekabidhi hundi ya Sh. bilioni 3.8 kwa ajili ya utoaji wa ruzuku kwa vyuo vilivyopo kwenye mradi wa kuendeleza ujuzi (SDF).

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, wakati wa kuzindua Mfuko huo wa kuendeleza ujuzi, uliofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa kushirikiana na serikali, Profesa Ndalichako, alisema lengo ni kuziwezesha taasisi zinazotoa mafunzo ya ufundi katika ngazi mbalimbali.

“Serikali inategemea kuwa fedha hizi zitatumika vizuri na kuwanufaisha watanzania wa kawaida, hasa wale wa vijijini, kupitia mafunzo haya ya ufundi na wataweza kupata stadi stahiki zitakazo wawezesha kupambana na mazingira yao,” alisema Profesa Ndalichako.

Alisema katika kutekeleza azma hiyo, wizara imeipa Mamlaka ya Elimu Tanzania (Tea), jukumu lakusimamia kipengele muhimu ndani ya huo cha Mfuko wa Maendeleo ya Ujuzi.

 Profesa Ndalichako alisema, Kupitia mfuko huo Tea watakuwa na jukumu la utambua taasisi ambazo zina uwezo wa kutoa mafunzo kwa sekta za kimkakati na kuziwezesha kutoa mafunzo hayo kwa vijana wa kitanzania ili waweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji na shughuli za kutoa huduma.

 Amesema anatarajia kuwa kupitia mfuko huo wizara itafikia malengo ya kuhakikisha kuwa mchango wa sekta binafsi katika kudahili wanafunzi wa vyuo vya ufundi ngazi ya kati unaongezeka kutoka asilimia 21 ya mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 25 mwaka wa 2020.

 Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya Elimu Tanzania Dk Erasmus kipesha amesema TEA ina  mamlaka kusimamia majukumu sita .

Aliyataja majukumu hayo kuwa ni pamoja na kufadhili miradi ya Elimu katika ngazi zote ili kuinua viwango cha ubora wa Elimu na upatikanaji wake kwa usawa kulingana na mipango na Sera  za kitaifa kwa lengo LA kukidhi mAhitaji kijamii.

Kuishauri serikali juu ya vyanzo vingine vya mapato kwa ajili ya mfuko wa Elimu na kutafut rasilimali kwa ajili mfuko wa Elimu ikiwa ni rasilimali fedha au vifaa pamoja na Kutayarisha na kitathmn Mara kwa Mara vigezo na taratibu za kutenga na kutoa fedha  za mfuko  wa Elimu kwa Ngazi  zote nchini.

Kufustilia na kuhakiki matumizi ya fedha za mfuko  zilizotolewa  kwa bodi mikopo,kamisheni ya vyuo vikuu na baraza la  Elimu ya ufundi.pamoja mj na kujenga ushirikiano  na na taasisi za ndani na nje nchi kwa lengo kuboresha elimu.

Pia amesema mamlaka imeshiriki katika hatua mbalimbali za uanzishwsji wa mfuko wa sdf unaenda sambamba na dira ya taifa 2025 ya kuwa na jamii iliyoelinika vyema na inayojifunza

"Tunatambua kuwa ufanisi wa SDF utachangia sana utekelezaji  wa ilani ya chama Katika kipindi 2015-2020 sekta za uzalishaji Mali kama kilimo,ufugAji,uvuvi,viwanda vikubwa na vidogo na huduma kiuchumi km vile miundombinu ya nishati ,uchukuzi na ujenzi zitaelekeza  mipango yao ktk kupunguza umaskini na kuanziadha ajira hususan kwa vijana” amesema.
  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa  Joyce Ndalichako akikabidhi Mfano wa Hundi kwa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA)  kwa ajili ya utoaji wa ruzuku kwa vyuo vilivyopo kwenye mradi wa kuendeleza ujuzi (SDF). 
 Mwenyekiti wa bodi wa TEA, Profesa Maurice Mbago akizungumza kuhusiana na utekelezaji wa fedha hizo katika kuendeleza ujunzi katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya wakuu wa vyuo na watendaji mamlaka za elimu zilizo chini ya Wizara ya Elimu.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...