Na Stella Kalinga, Simiyu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amepiga marufuku magari ya kubeba wagonjwa (Ambulance ) kubeba watu au kitu chochote tofauti na wagonjwa na akawaagiza Waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya kote nchini,  kusimamia matumizi ya magari hayo na kuhakikisha yanatumika kwa matumizi yaliyokusudiwa kwa mujibu wa mwongozo.

Waziri Ummy ametoa agizo hilo Julai 12, 2018 katika uzinduzi wa Mradi wa TUWATUMIE wenye lengo la kuunganisha jamii hasa zile zilizo mbali na vituo vya tiba, ambao umezinduliwa katika Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, kuunganisha jamii zinazoishi maeneo magumu kufikiwa  na mfumo wa Huduma za Afya ambao umelenga kupunguza vifo  vya mama na Mtoto mkoani SIMIYU.

“Nimesikitishwa sana na kitendo cha gari la kubebea wagonjwa la Halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara kubeba dawa za kulevya, ninakemea jambo hili kwa nguvu zangu zote na ninawataka waganga wakuu wa mikoa na wilaya kote nchini kusimamia matumizi ya magari ya kubebea wagonjwa “ alisema Waziri Ummy Mwalimu

“ Ni marufuku gari la kubebea wagonjwa kubeba kitu tofauti na mgonjwa, yeyote ambaye tumemkabidhi gari la kubebea wagonjwa tutamchukulia hatua kali pale ambapo atakiuka mwongozo wa matumizi ya magari ya kubebea wagonjwa, nalipongeza sana jeshi la Polisi kwa kuchukua hatua na ninamtaka Mkurugenzi wa Halmashauri husika kuwasimamisha kazi mara moja dereva na wote waliohusika na gari hilo kubeba mirungi” alisisitiza.

Akizundua mradi wa TUWATUMIE Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii, Waziri Ummy  amewashukuru  wafadhili  wa mradi huu Amref Health Africa Tanzania chini ya Ufadhili wa Serikali ya Ireland kupitia Shirika la Irish aid  ambao utatekelezwa kwa kushirikiana na Benjamin Mkapa Foundation na Halmashauri za Itilima na Misungwi(Mwanza) ukiwa na lengo la kupunguza vifo vya mama na Mtoto.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu akibonyeza kitufe ishara ya uzinduzi wa mradi wa TUWATUMIE wenye lengo la kuwatumia  Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kuunganisha jamii zinazoishi maeneo magumu kufikiwa  na mfumo wa Huduma za Afya , katika Wilaya ya Itilima, Mkoani Simiyu Julai 12, 2018.
 Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Donatus Weginah akiwasilisha tarifa ya Mkoa kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu mara baada ya kuwasili mjini Bariadi kwa ajili ya kuzindua mradi wa wa TUWATUMIE Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kuunganisha jamii zinazoishi maeneo magumu kufikiwa  na mfumo wa Huduma za Afya, katika Wilaya ya Itilima, Mkoani Simiyu Julai 12, 2018.
 Kutoka kulia Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Mhe. Daudi Nyalamu, Mbunge wa Itilima, mhe.Njalu Silanga na Mkurugenzi wa Benjamin Mkapa Foundation, Dkt. Hellen Senkoro wakiteta jambo wakati wa  uzinduzi wa  mradi wa wa TUWATUMIE Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kuunganisha jamii zinazoishi maeneo magumu kufikiwa  na mfumo wa Huduma za Afya, katika Wilaya ya Itilima, Mkoani Simiyu Julai 12, 2018.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu na Viongozi wengine wakiwa katika picha na Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii wanaotarajia kuhudumia Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, wakati wa uzinduzi wa Mradi wa TUWATUMIE wenye lengo kuwatumia Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kutoa huduma kwa jamii, uliofanyika katika Wilaya ya Itilima, Mkoani Simiyu Julai 12, 2018.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...