Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

WAZIRI wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe amemuagiza mkandarasi wa mradi wa barabara ya Nyakanazi Kabingo Nyanza road work  kuhakikisha ifikapo Agosti 30 mwaka huu kilometa 23 kati ya kilometa 50 za lami ziwe zimekamilika kwa kiwango cha lami.

Ametoa maagizo hayo jana wilayani Kakonko mkoani Kigoma wakati alipoanza ziara yake akitokea mkoani Geita ambapo alianza kwa kutembelea barabara hiyo inayounganisha mkoa wa Kigoma na mikoa mingine.

Mhandisi Kamwelwe amesema wananchi wa Mkoa wa Kigoma hawajawahi  kuona lami, hivyo wanashauku kubwa ya kuona barabara hiyo ya lami inakamilika na Rais amewaletea mradi huo lazima na wao wafaidi ndani ya utawala wa awamu ya tano na wao wapate barabara.

Amesema barabara hiyo imepitiliza muda kwani ilitakiwa iwe imekamilika na kwa sasa wataenda na mkandarasi huyo kwa kupeana muda wa kukamilisha kazi kidogo.Pia amewatala Kampuni ya Nyanza road work kumsimamia mtu waliomuajiri kufanya kazi usiku na mchana ilimradi ukamilike kwa wakati."Nimeanza kumkagua Nyanza road work sijaridhishwa na mradi  unavyoendelea.Mradi huu umeanza mwaka 2014  na ulitakiwa uwe umekamilika.

Aidha amesema tayari wametanganza zabuni ya mradi mwingine wa Kabingo hadi Nduta kilomita 89 baada ya mienzi miwili watasainiana mkataba na mkandarasi mwingine aanzie hapo.Amefafanua malengo ni  miaka miwili maeneo yote yaliyobaki mkoani Kigoma yatakuwa na wakandarasi  ili mkoa wa Kigoma ufunguke kwa kiwango cha lami.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amesema wananchi wanataka barabara iwepo na lami wamechoka vumbi kila siku, na  kuwataka wakandarasi kasi walioionyesha leo baada ya kusikia Waziri anakuja waendeleze kasi hiyo.

Waziri huyo amewasili jana mkoani Kigoma ambapo atakuwa katika ziara ya siku nne,ambapo akiwa mkoani hapo atatembelea barabara ya Nyakanazi Kabingo na Kasulu Kidahwe zenye wakandarasi pamoja na kutembelea bandari ya Kigoma na Uwanja wa ndege.
Waziri wa Ujenzi uchukuzi na mawasiliano Muhandisi Isack Kamwelwe (pichani kati) akitoa malekezo kwa Meneja mradi wa barabara ya Nyakanazi-Kabingo kutoka kampuni ya Nyanza Road Work Massimo Cartula kuhusiana na ujenzi wa barabara hiyo,kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala
 Ujenzi wa bara bara Nyakanazi-Kabingo ukiendelea kwa kusua sua,ambapo Waziri Ujenzi amutolea maagizo mazito kuhakikisha mradi huo
ifikapo Agosti 30 mwaka huu kilometa 23 kati ya kilometa 50 za lami ziwe zimekamilika kwa kiwango cha lami.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...