Na Karama Kenyunko,Globu ya jamii

MAHAKAMA  ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam leo imemtia hatiani na kumhukumu msanii Wema Sepetu kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela au kulipa faini ya Shilingi milioni mbili baada ya kupatikana na hatia  katika kesi ya kukutwa na  kutumia dawa za kulevya. 

Wema amelipa faini na kuachiwa huru. 

Mahakama imewaachia huru wafanyakazi wake Wema, Matrida Abbas na Angelina Msigwa,  aliokuwa akishtakiwa nacho baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao. Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba.

Akisoma hukumu hiyo leo Hakimu Mkuu  Simba amesema, upande wa Mashtaka umeweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa, mshtakiwa Wema alitenda kosa la kutumia na kukutwa na dawa za kulevya. 

Kabla ya kusomwa kwa Hukumu hiyo leo Julai 20 mwaka 2018, mashahidi upande wa mashtaka kupitia Wakili wake, Constantine Kakula waliwasilisha mashahidi 5 ambao wameweza kuthibitisha mashtaka pasipo kuacha shaka kuwa mshtakiwa Wema ametenda kosa.

Upande wa washtakiwa walitoa utetezi wao wakiongozwa na Wakili Albert Msando  na walipomaliza walifunga ushahidi wao na kufunga kesi yao. Pande zote ziliwasilisha hoja za majumuisho za mwisho na hatimaye kesi ikapangiwa tarehe ya hukumu, huku watuhumiwa wakijitetea wenyewe.
Wema na wafanyakazi wake hao walikuwa wakishtakiwa na kosa la kukutwa na kiasi kidogo cha madawa ya kulevya chini ya kifungu cha sheria namba 17 (1)(b) cha sheria inayodhibiti matumizi ya dawa za kulevya.

Walidaiwa kutenda kosa hilo Tarehe 4 February mwaka jana huko nyumbani kwao Kunduchi Ununio
 Pichani kulia Wema Sepetu akiwa na Mama yake wakiwa katika ukumbi wa wazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alipokuwa akisubiri kusomewa hukumu yake dhidi ya kesi inayomkabili ya matumizi ya dawa za kulevya 
 Wema Sepetu akiwa katika ukumbi wa wazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alipokuwa akisubiri kusomewa hukumu yake dhidi ya kesi inayomkabili ya matumizi ya dawa za kulevya.Wema Sepetu aliambatana na Mama yake pamoja na Ndugu,jamaa na marafiki zake.
Wema Sepetu akiwa na mama yake, ndugu jamaa na marafiki wakiwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...