*Kamanda wa Polisi aelezea tukio hatua kwa hatua...asema kabla ya kujiua aliandika ujumbe

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

KAMANDA wa Polisi Mkoani ya Mara Juma Ndaki amethibitisha kutokea kwa tukio la askari Polisi PC Nelson William G 3777 kujiua kwa kujipiga risasi kwasababu za wivu wa mapenzi. 

Akizungumza na Michuzi Blog kwa njia ya simu jana jioni hii Kamanda Ndaki amesema askari huyo amejipiga risasi leo saa 8:30 mchana akiwa eneo la kambi za Polisi alikokuwa anaishi. 

Amefafanua kabla ya kujipiga risasi ameacha ujumbe kuwa ameamua kujua kutokana  na wivu wa mapenzi kwa madai amekuwa hana mahusiano mazuri na mwanamke wake ambaye alikuwa ni mpenzi wake. 

Kamanda Ndaki amesema askari huyo kabla ya kuchukua uamuzi huo aliingia pia kwenye malumbano na mpenzi wake baada ya kwenda kwenye chumba cha mpenzi wake na kisha kuamua kuharibu mali alizonunua. 

Amesema baada ya tukio hilo la kuharibiwa mali mwanamke aliamua kwenda kutoa taarifa Polisi, kitendo ambacho askari William hakikumfurahisha kwani aliona kama amedhalilishwa. 

Hivyo akaona njia pekee ni kuchukua uamuzi wa kujiua na ilipofika muda huo akaamua kujiua kwa kujipiga risasi. Kamanda Ndaki alipoulizwa kama kuna mtu yoyote amekamatwa amejibu hakuna kwani askari ameacha ujumbe kuwa amejiua kwasababu hizo ambazo kimsingi ni wivu.

Amesema kwa sasa mwili wa askari huyo umehifadiwa chumba cha kuhifadhia maiti wakati taratibu za mazishi zikiendelea. 

Alipoulizwa kama askari huyo alikuwa akiishi pamoja na mpenzi wake huyo,Kamanda Ndaki amejibu hawakuwa wakiishi pamoja kwani mwanamke alikuwa ana chumba chake na askari alikuwa anaishi kambini. 
Barua ilioachwa na Marehemu 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...