Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

SHULE ya sekondari ya Seminari ya Kiislamu Al Muntazir kwa mara nyingine tena wamewakutanisha wanafunzi wa shule za Sekondari nchini na nje ya nchi kwa lengo la kufanya mashindano ya kujadili mada mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

Mjadala huo umepewa jina la "Mwalimu Nyerere Schools Invitational Debate Championships" ili kuwajenga na kuwaandaa wanafunzi hao kuwa wataalamu na wajuzi kwa miaka ijayo.Akizungumza na vyombo vya habari Mkuu wa shule ya Al Muntazir Reuben Kimani ameeleza kuwa mashindano hayo kwa shule za Sekondari na hiyo ni mara ya tatu yamefanyika yakihusisha washiriki zaidi ya 200.

Na hiyo ni kwa lengo la kuwafanya wawe na fikra pana kwa elimu ya chuo watakayoendelea nayo, ambapo ameeleza kuna shule kutoka Zimbabwe na Kenya na wenyeji Tanzania wakiwakilishwa na shule za Tusiime, Shaaban Robert, shule ya wavulana na wasichana Feza, Aghakan na wenyeji Al Muntazir.

Aidha ameeleza kuwa mashindano hayo yatachukua siku 3 wale watakaofanya vizuri watatunukiwa vyeti na watashiriki mdahalo mkubwa utakaofanyika Desemba mwaka huu nchini Botswana. Kuhusiana na maandalizi kwa wanafunzi wao Kimani ameeleza kuwa wametoa mafunzo kwa wiki mbili yakihusisha utafiti hivyo hawana shida kwa shindano hilo na amewataka wanafunzi kuja kujishiriki kwa kutazama na kupata uzoefu kutoka kwa wanafunzi kutoka barani Afrika.

Mwalimu na mlezi wa klabu ya Lugha ya kiingereza kutoka Al Muntazir Seminari Bi. Getrude Mtenga akieleza namna shule yao ilivyojipanga katika kukabiliana na mashindano hayo.
Mkuu wa shule ya Sekondari ya Seminari ya Al Muntazir, Reuben Kimani akitoa neno kwa washiriki kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.
Baadhi ya wanafunzi walioshiriki mdahalo huo kutoka shule za sekondari nchini.
Wanafunzi kutoka Zimbabwe (wenye suti za bluu) wakisikiliza mjadala uliokuwa unaendelea.KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...