Na Jumia Travel Tanzania

Ushawahi kukumbana na kadhia ya kunyimwa huduma ya malazi? Au kulipishwa kwa kutozingatia masharti ya hoteli kuhusu huduma zao?

Wasafiri wengi siku hizi hufanya maandalizi ya mapema pindi wanapotaka kusafiri. Lengo la kufanya hivi linaweza kuwa kupata bei nzuri zaidi au kuepuka usumbufu wa maandalizi ya dakika za mwisho. Lakini kwa baadhi yetu, kufanya maandalizi ya namna hiyo huona kama ni kujisumbua tu kwa sababu kuna uwezekano wa kuahirisha safari yenyewe.

Unaweza kuona kuwa ni jambo la kawaida wewe kama mteja kuamua kuahirisha safari yako na kuwaambia hoteli wasitishe huduma ya malazi uliyoweka. Lakini kuna masuala muhimu ya kuzingatia kuhusu sera zinazowekwa na hoteli hususani katika kusitisha huduma ya chumba ambayo Jumia Travel ingependa kukupatia ufahamu. 




Kuna umuhimu kwa wasafiri kuzifahamu sera za hoteli husika ukizingatia kumekuwa na mitandao mingi iliyoibuka kwa kasi katika utoaji wa huduma za malazi. Ushauri wa kwanza, msafiri anashauriwa pindi anapofikiria kusitisha huduma ya chumba hotelini aliyoifanya ni kujaribu kusoma kwa makini sera za hoteli ili kufahamu kwamba hatohitajika kulipia gharama zaidi pale atakapoamua kusitisha huduma.


Mambo muhimu ya kuzingatia

Endapo utakuwa umefanya huduma ya malazi ya chumba hotelini moja kwa moja utakuwa na faida mbili:

Kwanza, kama umeenda hotelini moja kwa moja na kufanya huduma kwa utaratibu uliozoeleka unaweza kuwa na faida ya kusitisha huduma yako hata masaa 24 kabla ya kuripoti. Utaratibu huu unaweza kukupa faida ya kurudishiwa takribani pesa zako zote kama ulishalipa au hautokatwa chochote kama hautokuwa umelipa. Mara nyingi njia hii ni rahisi na huwa haina matatizo.

Pili, kama utakuwa umefanya huduma ya malazi ya kabla basi ujue suala la kusitisha huduma kwako litakuwa ni changamoto kwako. Hii ni kutokana na sababu ya kwamba kwa mtazamo wa hoteli, utakuwa umepewa ofa ya bei nzuri tofauti na wengine na hawatokuwa tayari kukuachia uende kirahisi. Ukiachana na kufanya huduma ya malazi moja kwa moja hotelini, siku hizi kuna njia za kufanya huduma kupitia mitandao mbalimbali.

Mfumo wa kufanya huduma za malazi kwa njia ya mtandao unakupatia fursa ya kuperuzi na kulinganisha huduma za hoteli mbalimbali kwa urahisi na wakati mmoja. Faida ya kutumia mitandao kama hii ni kwamba mingi miongoni mwao huonyesha sera za hoteli katika kusitisha huduma ya malazi uliyoifanya.

KUSOMA ZAIDI  BOFYA HAPA>>>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...