SERIKALI ya awamu ya tano imeombwa kuangalia namna ya kuanza ujenzi wa barabara ya Tanga-Pangani, Saadan hadi Bagamoyo ili kuweza kumaliza kilio cha wananchi wa wilaya ya Pangani cha muda mrefu ikiwemo kufungua fursa za kiuchumi na maendeleo kwa mkoa . 

Ombi hilo lilitolewa na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso wakati akizungumza kwenye mkutano wake wa hadhara wilayani humo ambapo alisema pamoja na kuwepo kwa miradi mingi inayotekelezwa huko lakini kilio kikubwa cha wananchi wake ni ukosefu wa barabara nzuri. 

Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) alisema wakati Rais Magufuli akiomba kura kwa wananchi hao mwaka 2015 aliwaahidi wananchi ujenzi wa barabara hiyo na walikubali kumpa kura nyingi na imani kubwa kwake kwa mategemeo ya kumpata mkombozi atakae weza kumaliza kero hiyo ambayo imedumu katika awamu zote nne zilizopita bila ya mafanikio. 

“Kwenye mkutano wangu wa leo hii nipo hapa nyumbani kama Mbunge wenu kawaida na sikuja kama Naibu Waziri na jukumu la Mbunge ni kuwasemea wananchi wake Mh Rais wananchi wangu kiukweli wanalia na suala la barabara hii na hawajui hatma yake lini mradi huu utaanza”Alisema Aweso. 

Hata hivyo alisema kuzorota kwa uchumi na maisha magumu kwa wananchi wa wilaya hiyo unachangiwa kwa kiasi kikubwa na tatizo la kutokujengwa barabara ambayo ingesaidia kufungua wilaya hiyo ambayo inaonekana kama imesahaulika katika nyanja zote. 
 NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) akizungumza na wananchi wa Jimbo hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika sokoni mjini Pangani ambako pamoja na mambo mengine aliweza kusikiliza kero zao zinazowakabili
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) akiwa amebebwa juu na wananchi mara baada ya kumaliza kuwahutubia
 NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)kulia akiwa na Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa Abdallah wakifuatilia hoja za wananchi kwenye mkutano huo
sehemu ya wananchi wa mji wa Pangani wakimfuatilia NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)
Wananchi wakimfuatilia NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...