WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania bado inawahitaji wawekezaji zaidi katika sekta ya uzalishaji wa sukari ili iweze kukidhi mahitaji. 

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Mauritius nchini Tanzaniamwenye makazi yake Maputo nchini Msumbiji, Mheshimiwa Jean Pierre Jhumun, ofisini kwake jijini Dodoma. 

“Mwaka jana nilikiwa nchini Mauritius nilihudhuria Jukwaa la Wafanyabiashara na Wawekezaji kati ya Tanzania na Mauritius, ambapo nilipata fursa ya kuwashawishi wawekezaji wa Mauritius waje kuwekeza kwenye viwanda vya sukari nchini,”. 

Ameongeza kuwa Tanzania ina fursa kubwa ya maeneo ya uzalishaji wa sukari ambayo bado hayajaendelezwa, hivyo kama kuna wawekezaji walio tayari na wamekidhi vigezo waendelee na hatua za uzalishaji. 

Waziri Mkuu ameongeza kuwa mbali na kuhitaji wawekezaji kwenye sekta ya sukari, pia amewakaribisha wawekezaji kutoka nchini Mauritius kuja kuwekeza kwenye sekta ya uvuvi. “Mnaweza kuja kuwekeza kwenye viwanda vya usindikaji wa samaki kwani tuna bahari, mito na maziwa yenye samaki wa aina mbalimbali,” 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Mauritus nchini mwenye makazi yake, Maputo nchini Msumbiji, Jean Pierre Jhumun, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dodoma, Agiosti 15, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Mauritius nchini mwenye makazi yake Maputo nchini Msumbiji, Jean Pierre Jhumun (wapili kushoto) Balozi wa Heshima wa Mauritius nchini, Kazim Rizvi (kulia), Mwenyekiti wa Mfuko wa Uwekezaji Sukari nchini Mauritius, Gansam Boodram (wapili kulia) na kushoto ni Mwenyeji wa ujumbe huo katika jiji la Dodoma, Kapteni Mstaafu John Chiligati. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Mauritius nchini mwenye makazi yake Maputo nchini Msumbiji, Jean Pierre Jhumun (wapili kulia) na ujumbe wake, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dodoma Agosti 15, 2018. Wengine kutoka kushoto ni Balozi wa Heshima wa Mauritius nchini, Kazim Rizvi, Mwenyekiti wa Mfuko wa Uwekezaji Sukari nchini Mauritius, Gansam Boodram na watatu kushoto ni Mwenyeji wa ujumbe huo katika jiji la Dodoma, Kapteni Mstaafu John Chiligati. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...