Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al-Najem ametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kuahidi kuwasaidia watoto wenye saratani ambao wanatibiwa katika hospitali hiyo.

Katika ziara hiyo balozi huyo alimtaka Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tumaini la Maisha (TLM) katika hospitali hiyo, Dkt. Trish Scanlan kumwandikia mahitaji ambayo watoto hao wanapaswa kupatiwa ili aweze kushiriki katika kuwapatia tiba pamoja na mambo mengine. 

Balozi huyo aliongozana na Naibu Mwenyekiti wa Red Crescent kutoka Kuwait, Anwar Alhasawi, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati-Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki , Suleiman Salehe pamoja na pamoja na viongozi mbalimbali wa Lions Club ambayo imekuwa ikiwasadia watoto hao mahitaji mbalimbali.

Pia, balozi huyo alitembelea watoto wenye saratani katika jengo la watoto pamoja na kuwapatia zawaidi mbalimbali ikiwamo vifaa vya kuchezea.
Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa mwezi imekuwa ikipokea wastani wa watoto 30 hadi 40 wenye saratani ya aina mbalimbali. Wengi wa watoto wanaopokelewa wamekuwa wakisumbuliwa na saratani ya damu, jicho, figo na saratani ya matezi.
 Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al-Najem akimkabidhi zawadi mmoja wa kina mama, Martha John Zakaria anayemuuguza mtoto wake katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Kushoto ni Naibu Mwenyekiti wa Red Crescent kutoka Kuwait, Anwar Alhasawi na mwakilishi wa Jumuiya ya Red Crescent, Mayouf Alenezi.
 Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al-Najem akizungumza na wazazi wa watoto ambao wanatibiwa saratani katika hospitali hiyo. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati-Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Suleiman Saleh na Naibu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Red Crescent kutoka Kuwait, Anwar Alhasawi.
 Wazazi na watoto wakimsikiliza balozi huyo katika jengo la watoto.
 Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al-Najem akizungumza na Ofisa Mtendaji wa Tumaini la Maisha (TLM), Dkt. Trish Scanlan  baada ya ofisa huyo kumweleza mahitaji wanahitaji watoto wanaotibiwa saratani katika hospitali hiyo.  Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati-Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Suleiman Saleh, kulia ni Naibu Mwenyekiti wa Red Crescent kutoka Kuwait, Anwar Alhasawi (mwenye koti) na wengine ni wawakilishi wa Jumuiya ya Red Crescent.
Balozi huyo akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto baada ya kupewa zawadi mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...