*Yazindua huduma ya Klik App NMB inayowezesha kufungua akaunti kupitia simu ya mkononi

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imeipongeza Benki ya NMB kwa uamuzi wake wa kuzindua huduma ya kufungua akaunti kwa kutumia mtandao wa simu ya mkononi.Imesema hatua hiyo imethibitisha namna benki hiyo inavyotumia ubunifu na kukua kwa teknelojia ya mawasiliano kwa kurahisisha huduma za kibenki nchini.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Gavana Usimamizi wa Fedha Benki Kuu ya Tanzania(BoT)Dk.Benard Kibese wakati akizindua Klik App ya NMB inayowezesha mteja kufungua akaunti kupitia simu ya kiganjani.

Amesema kuwa ubunifu huo ambao umefanywa na benki ya NMB utarahisha watanzania wengi kufungua akaunti za benki hiyo kupitia simu zao na kwamba hivi sasa watumiaji wa simu za mkononi ni wengi na hivyo huduma hiyo ya NMB imekuja wakati sahihi.

“Tunaipongeza NMB kwa ubunifu huu ambao wamekuja nao wa kuhakikisha wanatumia teknolojia iliyopo kuanzisha huduma za kufungua akaunti kupitia simu ya mkononi na kizuri zaidi hata wenye simu za tochi bado wanaweza kufungua akaunti kupitia huduma hiyo,”amesema Dk.Kibese.

Amefafanua kuwa kama mnavyofahamu idadi kubwa ya Watanzania wanapotaka kununua bidhaa wanakwenda na fedha mkononi na hiyo imekuwa changamoto kubwa hasa ya usalama wa fedha.Lakini sasa NMB mbali ya kuja na huduma ya kukuwezesha kufungua akaunti kwa kutumia simu ya mkononi pia wanayo huduma nyingine ambayo inakuwezesha kununua bidhaa kwa kutumia simu.
Naibu Gavana Usimamizi wa Fedha Benki Kuu ya Tanzania(BoT)Dk.Benard Kibese akizungumza wakati wa uzinduzi wa uzinduzi wa huduma ya kibanki ya NMB inayojulikana kwa jina la Klik App ya NMB kwenye hoteli ya Hyyat jijini Dar es salaam leo.
Bi. Ineke Bussemaker Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NMB akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo kwenye hoteli ya Hyyat jijini Dar es salaam.
Naibu Gavana Usimamizi wa Fedha Benki Kuu ya Tanzania(BoT)Dk.Benard Kibese akiwa amekaa pamoja na wageni mbalimbali waalikwa na viongozi wa benk ia NMB wakati wa hafla ya uzinduzi huo.
Baadhi ya wakurugenzi wa vitengo mbalimbali Benki ya NMB wakiwa katika hafla hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...