Bendi maarufu ya Muziki wa dansi barani ulaya The Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni ukipenda waite viumbe wa ajabu Anunnaki au "Watoto wa Mbwa" inayoongozwa na kamanda Ras Makunja inatarajiwa kulitingisha jukwaa la Alafia Festival katikani ya jiji la Hamburg katika viwanja vya hamburg-Altona Ujerumani siku ijumaa tarehe 24-08-2018 kuanzia majira ya saa 2.00 usiku (20.00 hour)
Bendi hiyo maarufu inayodumu kwa miaka 24 sasa katika majukwaa ya kimataifa na mtindo wake wa "Bongo Dansi made in Uswahilini"  inazidi kuwanasa washabiki katika kila pembe barani ulaya,ni juzi kati tu ilitumbuiza katika onyesho kubwa mjini Tuebingen,Ujermani na Mamling Festival nchi Austria,na ijumaa ya tarehe 24 Augosti 2018 watatingisha tena mjini Hamburg-Altona.
Usikose kuungana nao katika tamasha hilo la wazi pia unaweza kujumuika nao mubashara at www.facebook.com/ngomaafricaband 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...