Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Kagera, Agustino Allomi amesema kwa sasa wanaendelea na jitihada za kuzima moto ambao umetokea baada ya magari mawili kugongana wilayani Ngara.

Moto huo umeanza kuwaka saa tatu asubuhi na bado unaendelea hadi muda huu wa mchana kwa mujibu wa Kamanda Olomi na kufafanua juhudi za kuuzima zinaendelea na kunamatumaini ya kufanikiwa kuudhibiti moto huo.

Akizungumza na Michuzi Blog kwa njia ya simu Kamanda Olomi amethibitisha tukio la kutokea kwa moto huo baada ya gari mmoja kugongana magari mengine eneo la Rusumo.

Kamanda Olomi amesema cha kwanza wanachokifanya ni kuuzima moto huo na kisha watafanya uchunguzi wa chanzo cha moto huo kwani ni mapema kuzungumzia cha moto ingawa ulianza baada ya gari moja kugonga mengine yaliyokuwa eneo hilo.

"Tutatoa taarifa rasmi ya chanzo cha moto huo,kwa sasa tunaendelea kuuzima.Ni tukio la kushangaza maana eneo hilo magari kila siku yapo na yanapita,hivyo lazima tufanya uchunguzi kubaini ukweli wa chanzo cha  moto, huo" amesema Kamanda Olomi.

Alipoulizwa moto huo ulianza kuwaka saa ngapi amejibu ulianza kati ya saa tatu na nusu na saa nne kasoro asubuhi na juhudi za kuendelea kuuzima unaendelea.

Awali Michuzi Blog ilitoa taarifa za awali kuhusu kuungua moto kwa magari katika eneo la Rusumo jirani na Ofisi za  Idara ya Uhamiaji ambazo zipo mpakani kwa Tanzania na Rwanda.

Hivyo kadri muda unavyokwenda tutaendelea kuwajuza wasomaji wa Blog makini ya Michuzi Blog.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...