Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

MKUU wa Wilaya Ilala, Sophia Mjema, ameagiza Taasisi ya Kuzuia ya Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kuchunguza kamati ya mradi wa ulasimishaji ardhi katika Kata ya Kipunguni B kutokana kuwepo viashiria vya ubadhirifu wa fedha za wananchi katika mradi huo .

Dc Mjema alitoa agizo hilo, Kipunguni wilayani Ilala, jana wakati akipokea kero kutoka kwa wananchi wa eneo hilo, wakidai kuchangishwa fedha kulipia gharama za mradi huo.Wananchi wamedai kuchangishwa Sh. 50,000 kwa utambuzi na Sh. 400,000 na kamati hiyo inayojulika vinondo kwa ajili ya kupimiwa ardhi warasimishiwe makazi yao ikiwemo kupatiwa hati miliki.

Mjema alisema sheria iliyoko ni kwamba wananchi walipishwe Sh.250,000 tu, kwa ajili huduma hiyo kutoka katika kampuni ambazo ziko kisheria."Suala hili naiagiza TAKUKURU ilifanyie kazi kwa kuifanyia uchunguzi kamati hiyo, ikibainika sheri aichukue mkondo wake, lakini utaratibu ni kwamba kampuni yeyote itapima kwa Sh. 250,000 tu si zaidi ya hiyo", alisema Mjema.

Kuhusu kero ya elimu ya baadhi ya shule za kata hiyo kukosa uzio, amemuagiza Mkurugenzi wa Wilaya kuhakikisha shule hizo zinawekewa uzio haraka.Pia ameagiza kuchukuliwa hatua kwa mwalimu wa Shule ya Msingi Kipunguni B, baada kumwambia mzazi wa mmoja wa wananfunzi wazazi wao wandamane kama anaona watoto wao hawaelewi masomo.

Kero hiyo iliwakilishwa na mmoja mkazi wa Kipunguni B, aliedai kuambiwa na mwalimu wa shule hiyo, baada kuhoji kwa mwalimu huyo kuwa mtoto wake maendeleo yake si mazuri darasani.Alisema mwalimu huyo atafutwe na achukuliwe hatua za kisheria kwa kuhamasisha hayo maandamano kwani jukumu la mwalimu kufundisha sio kutaka watu waandamane.

"Naagiza kwamba ofisa wa elimu, akamtafute huyo mwalimu aliyetoa kauli hiyo kwa wanafunzi, awamu hii ya serikali ni kufanya kazi kwa wananchi", alisema.Pia, Mjema kuhusu kero ya kupandishwa kwa nauli dalala kiholela kutoka kituo cha Mombasa hadi Kipunguni, kuwa atafanya kikao kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usafiri nchi Kavu na Majini (SUMATRA) na mwakilishi wa wananchi ili kupata usahihi wa nauli hiyo.

Alisema haiwezekani kila wakati nauli ziwe zinapandishwa kwa wananchi, na hiyo imekuwa tabia ya baadhi dalala kuwa barabara ikichimbika kidogo wanapandisha nauli hilo halitawekana.Kuhusu mikopo kwa vijana na wanawake, amewataka kujiunga katika vikundi ili wajiandikishe kwa mtendaji ili wapewe mikopo.

Alisema hiyo ni fursa wanapaswa kuichangamkia kwani ni fedha za serikali zipo kwa ajili yao ili waweze kujipatia maendeleo na miradi iko mingi kufanya.
Mkuu wa Wilaya Ilala Sophia Mjema akizungumza katika eneo la mradi kilipochimbwa kisima cha maji ambacho wananchi wamekilalamikia kuwa hakina tija.
Mkuu WaWilaya Sophia Mjema akikagua Msingi wa Zahanati ya Kipunguni B ambao umekaa kwa zaidi ya miaka mitatu bila kujengwa 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...