NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Dk.Bashiru Ally amezitadharisha baadhi ya nchi za kigeni kuacha tabia ya kuingilia siasa za ndani ya nchi.

Amesema lazima nchi hizo hasa zenye balozi Tanzania ziheshimu Katiba na miongozo ya kisheria ya nchi, vinginevyo Tanzania itashindwa kuvumilia uchochezi unaofanywa na baadhi ya balozi nazowakilisha nchi hizo Tanzania.

Hayo ameyasema leo wakati akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM katika viwanja vya Afisi kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar makuu, Dk. Bashiru amesisitiza kuwa Tanzania ni taifa huru linalojitawala lenyewe na hakuna nchi yoyote itakayoweza kuyumbisha demokrasia ya nchi hiyo.

Amesema kumejitokeza baadhi ya mataifa yanayojifanya viranja wa demokrasia ambayo yamekuwa na tabia ya kutoa matamko ya kuhusu ushindi wa CCM wakati haijasajiliwa kufanya kazi za kisiasa. Katibu Mkuu huyo ameeleza kuwa katika siku za hivi karibuni kumetokea taifa moja la kibeberu linatuma matamko kwenye mitandao ya kubeza ushindi wa CCM hivyo wanatakiwa waheshimu utawala na demokrasia ilioko nchini.

Dk.Bashiru amefafanua kuwa hakuna taifa lenye haki ya kubeza ushindi wa CCM inaoupata katika chaguzi ndogo zinazofanyika nchni, kwani kufanya hivyo ni kuingilia siasa za ndani za taifa hili. Katika maelezo yake amebainisha kwamba kinachotakiwa kitambulike ni kuwa CCM haitishwi na matamko ya aina hiyo ya kuibeza na kwamba hawache kuidharau.


Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi Taifa Ndugu Abdallah Haji Haidar ambaye ni mmoja kati ya viongozi mbali mbali walioshiriki katika mapokezi hayo.


KATIBU Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally, akiwa na viongozi mbali mbali wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali wakipokea maandamano ya vijana na Wana-CCM walioshiriki katika mapokezi hayo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...