Na Benny Mwaipaja, WFM, Kigoma.

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmahauri ya Wilaya ya Kigoma kumrejesha mara moja katika kituo chake cha kazi cha awali, dereva wa Kituo cha Afya Bitale, kilichoko Kata ya Bitale katika Halmashauri ya wilaya hiyo baada ya kubainika kuwa gari la kubeba wagonjwa kituoni hapo halina dereva.
Dkt. Kijaji, ametoa maelekezo hayo alipotembelea Kituo hicho cha Afya kukagua ujenzi wa majengo mapya ya Kituo hicho yatakayogharimu shilingi 400m  baada ya Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Bitale, Dkt. Norbert Nshemetse, kueleza changamoto ya upungufu wa watumishi wa kituo hicho akiwemo dereva.
Dkt. Nshemetse, pamoja na kumshukuru Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, kwa kuwapatia gari la wagonjwa (Ambulance) katika kituo hicho, alisema gari hilo halina dereva baada ya dereva wake kuhamishiwa katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma mwezi Julai, 2018.
“Katika jambo lililonishitua ni kupata taarifa kwamba dereva aliyekuwa akiendesha gari la wagonjwa hapa Kituoni amehamishwa kupelekwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wakati anahitajika zaidi hapa kuliko huko kwa Mkurugenzi” alisikitika Dkt. Kijaji
 AC3A7908
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akitoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Kigoma, kumrudisha Dereva wa gari la Kituo cha Afya cha Bitale ambaye alihamishiwa katika Ofisi ya Mkurugenzi na kukifanya kituo hicho kukosa huduma za gari kwa wagonjwa, kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Uvinza na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bi. Mwanamvua Mlindoko, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo Mkoani Kigoma.
AC3A7887
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kulia)  akipokea taarifa ya Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya  Bitale kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho Wilayani Kigoma Mkoani Kigoma, Dkt. Norbert Nshemetse, wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea na kukagua maendeleo ya mradi huo utakaogharimu takribani Sh. milioni 400 hadi kukamilika kwake.
AC3A7881
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Bitale Wilayani Kigoma, mkoani Kigoma, Dkt. Norbert Nshemetse akisoma taarifa ya Mradi wa Ujenzi wa miundombinu ya Kituo hicho likiwemo jengo la Wazazi, Mionzi na Kliniki  ya mama na mtoto ambapo tayari Sh. Milioni 400 zitatumika kwa kazi hiyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...