Benny Mwaipaja, Kakonko, Kigoma

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amewashauri wakazi wa Wilaya ya Kakongo na mkoa wa Kigoma kwa ujumla kuchangamkia fursa za biashara kati ya mkoa huo na nchi jirani za Rwanda na Burundi kwa kuuza mazao ya kilimo yaliyochakatwa likiwemo zao la muhogo ili waweze kunufaika na biashara hiyo ya mipakani.

Dkt. Kijaji ametoa rai hiyo mjini Kakonko baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na wafanyabiashara wa wilaya hiyo, mkutano uliolenga kujadili fursa na changamoto za ufanyaji biashara katika eneo hilo yakiwemo masuala ya kikodi.

"Nakuomba Mkuu wa Wialaya ya Kakonko uwakutanishe na kuwaunganisha wafanyabiashara hawa ambao nafurahi wengi wao ni vijana ili waandae andiko la namna ya kununua mashine za kuongeza thamani ya mazao ili wauze nje yakiwa yamechakatwa badala ya mfumo wa sasa ambao wanauza mazao ghafi nje ya nchi na hivyo kupata hasara" alisisitiza Dkt. Kijaji

Awali, wafanyabiashara wa Kakonko walimweleza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu kijaji, aliyeambatana na Kamishna wa Mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Bw. Elijah Mwandumbya, kwamba, bei ya zao la muhogo imeshuka kutoka shilingi 600 kwa kilo katika msimu uliopita hadi kufikia shilingi 150, hali iliyowasababishia wakulima maumivu makubwa.

"Wafanyabiashara wanaonunua mazao yetu kutoka Burundi ni watu wa kati kwa maana ya madalali ambao wananunua mazao yetu kwa bei nafuu na kuyapeleka n hini kwao ambako huyachakata na kuyauza kwa bei kubwa nchini mwao na nchi za Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya kongo, hivyo tunaiomba Serikali itupatie mikopo kupitia Benki ys Kilimo ili tusnzishe viwanda vya kuchakata mazao yetu" alieleza mfanya biashara Dkt. Brighton Gwamagobe

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (katikati), akiwaasa wafanyabiashara wa Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma (hawapo pichani) kutumia fursa zilizopo katika nchi jirani ikiwemo Burundi kuuza bidhaa zilizoongezwa thamani ili kukuza uchumi wa Wilaya hiyo, alipofanya mkutano na Wafanyabiashara hao Wilayani hapo, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala, na kulia ni Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Kakonko Bw. Kadudusi Bunabuna.

Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA anaye husika na kodi za, ndani Bw. Elijah Mwandumbya, akifafanua masuala mbalimbali ya kikodi kwa wafanyabiashara wa wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma, wakati Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji alipokutana na wafanyabiashara hao kujadili fursa na changamoto wanazopata.


Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala, akizungumza na wafanyabiashara wa Wilaya hiyo wakati wa Mkutano kati ya Wafanyabiashara hao na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani).

Mfanyabiashara wa Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma Bw. Musa Ndiliwe, akieleza kuhusu kuimarishwa kwa mazingira bora ya kibiashara katika Soko la Ujirani mwema kati ya yao na wenzao wa Nchini Burundi kwa lengo la kukuza biashara, wakati wa mkutano kati ya wafanyabiashara hao na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) Wilayani hapo.

Maafisa wa Wizara ya Fedha na Mipango walioko kwenye msafara wa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, wakifuatilia mkutano kati ya Serikali na wafanyabiashara wa wilaa ya Kakonko mkoani Kigoma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...