Na Benny Mwaipaja, WFM, Mtwara

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameuahidi uongozi wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo Naliendele kwamba Serikali itakiwezesha Kituo hicho na vituo vingine vya utafiti nchini ili viendeleze kazi ya utafiti wa mazao ya kilimo ambacho kinategemewa na watanzania wengi katika kujikwamua kiuchumi.

Dkt. Mpango ametoa ahadi hiyo alipotembelea Kituo cha Utafiti Naliendele, mkoani Mtwara, ambacho uongozi wake ulielezea wasiwasi wake wa kupata rasilimali fedha za kuendeleza utafiti wa mazao likiwemo zao la korosho pamoja na watumishi baada ya kuondolewa kwa fedha za ushuru wa korosho inayouzwa nje, zilizokuwa zikitumika kuendeleza utafiti huo.

Alisema kuwa Serikali inatambua umuhimu wa shughuli za utafiti katika kuendeleza uchumi na maendeleo ya nchi kwa ujumla na kwamba atajitahidi kama Waziri wa Fedha na Mipango kwa kushirikiana na Waziri mwenzake anayeshughulikia kilimo ili taasisi hiyo isikwame kufanya shughuli zake.

"Niwahakikishie kabisa kwamba Serikali haitakubali utafiti wa mazao yote unaofanyika hapa likiwemo zao la korosho udhurike, litakuwa ni janga kubwa, kwahiyo upatikanaji wa fedha za Kituo hiki litakuwa ni moja ya vipaumbele vyangu" alisisitiza Dkt. Mpango

Alisema kuwa kilimo ndiyo uti wa mgongo wa Taifa na kwamba hakutakuwa na mapinduzi ya viwanda bila kilimo kwa sababu viwanda vinavyojengwa vinatarajiwa kuongeza thamani ya mazo ya kilimo pamoja na mazao ya mifugo na uvuvi.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akipata maelezo kuhusiana na zao la Korosho,alipotembelea Kituo cha Utafiti Naliendele, mkoani Mtwara
Mmoja wa Wataalamu pichani juu na chini kutoka kituo cha Utafiti Naliendele akifafanua jambo mbele ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango alipotembelea Kituo cha Utafiti Naliendele, mkoani Mtwara

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...