JOSEPH MPANGALA -MTWARA.

Serikali imesema Imefuta Mpango wa Kufanya Elimu ya Msingi Kuishia darasa la Sita Kutokana na Kuonekana Mfumo wa Kuishia Darasa la Saba Hauna matatizo Yoyote na Umeendelea Kufanya Vizuri kwa Wanaomaliza.

Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha mara baada ya Kumaliza kutembelea Chuo cha Ualimu Kitangali Kilichopo Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara.Ole Nasha Amesema Mpango wa Elim ya Msingi Kuishia darasa la Sita Ulikuwepo lakini baada ya Kupokea mawazo Wameamua Kuacha kama Ilivyo.

“Kulikuwa na Mpango wa kujaribu kufanya sasa Elimu ya msingi iishie darasa la Sita iwe miaka sita lakini kwa sasa hakuna huo Mpango tumerudi kwenye mfumo wetu wa kawaida kwa sababu moja tu hakuna kitu kilicho haribika, kila mtu aliyesoma Nchi hii amesoma kwa mfumo ule hatujaona kama unamapungufu yoyote kwa hiyo tutaendelea na utaratibu wetu wa Miaka Saba”amesema Ole Nasha

Aidha Naibu waziri amewataka Makandarasi wanaojenga Katika Mradi wa Chuo Cha Kitangali Kuhakikisha wanamalizia Ujenzi Pindi watakapo pata Pesa Kutoka serikalini.

“Mimi ninaloondoka nalo hapa ni kwenda kuhakikisha kwamba Fedha Yaani Certificate hizo ambazo zimetoka karibuni kwamba zinalipwa mapema, Rai yangu kwenu Jamani Mradi huu umechukua muda mrefu,karibia miaka miwili kwa hiyo fedha zikilipwa kila mmoja ajitahidi huu Mradi sasa uishe na ukabidhiwe ili lengoletu lile na chuo kuweza kudahili Wanafunzi wengi zaidi Liweze Kufikia”Amesema Ole Nasha..

Mradi wa Ujenzi wa Chuo cha Ualimu kitangali Unagharimu Shilingi billioni 8 lakini mpaka sasa Wakandarasi wamekwisha Pewa Shilingi Billion 3.2 jambo ambalo limepelekea Mradi huo Kuchukua Miaka 2 Kushindwa Kumalizika.
Kulia Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiwa na Mkuu wa Chuo Cha mafunzo ya Ufundi Stadi VETA Mtwara Samweli Kibehele wakati wa ziara ya kutembelea Chuo hicho kwa lengo la kutazama mazingira yanayotumika kufundishia Wanafunzi wa VETA. 
Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akipewa maelezo ya Mradi wa Ujenzi wa Chuo Cha Ualimu Kitangali na Mshauri wa Ujenzi Nicodemus Mgaya katika ziara yake ya kutazama Maendeleo ya Ujenzi Huo.
Naibu waziri wa Elim Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha Akiongea na wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchii FDC ambacho kimeanzishwa mwaka 1975 ambacho kinafundisha masomo ya Umeme,Ufundi wa Magari pamoja na Ushonaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...