Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MICHUANO ya Sprite Bball Kings 2018 imefikia hatua ya fainali baada ya timu za Flying Dribblers na Mchenga Bball Stars kushinda mechi zao za nusu fainali.

Msimu wa pili wa mashindano ya Sprite Bball Kings 2018 ulizinduliwa Juni 11 mwaka huu katika Viwanja vya Mlimani City Mall na jumla ya timu 51 na zikiwa na jumla ya washiriki zaidi ya 510 kutoka pande mbalimbali Tanzania walijisajili na kushiriki michuano hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Vipindi wa EA Radio, Nasa Kingu amesema kuwa michuano hiyo ilianza rasmi Juni 30 kwa timu 51 kucheza hatua ya mtoano na kupatiakana kwa timu 16 zilizoingia hatua iliyofuata.

Kingu amesema kwa sasa mashindano ya Sprite Bball Kings 2018 yamefikia hatua ya fainali na timu ya Flying Dribblers pamoja na timu ya Mchenga Bball stars zitachuana vikali kuwania ubingwa mechi hizo zikiwa katika Game 5.

Ameeleza kuwa, timu ya Mchenga Bball stars ndiye bingwa mtetezi akiwa na kumbukumbu ya kumtoa mpinzani wake Flying Dribblers hatua ya nusu fainali msimu uliopita na sasa hivi wanakutana katika hatua ya fainali.

Fainali za mashindano ya Sprite Bball Kings 2018 yanatarajiwa kuanza rasmi  Jumamosi Agosti 18 - Game 1 utakaochezwa katika Uwanja wa ndani wa Taifa , jumatano Agost 22 - Game 2 katika Viwanja vya Don Bosco, Jumamosi Agost 25- Game 3 Uwanja wa Ndani wa Taifa na kama italazimika kuendelea na game 4 na 5, mechi hizo zitachezwa Jumamosi  Agosti 29 Game 4 na Jumatano Septemba  01- Game 5 na mechi hizo zitachezwa katika Viwanja vya  Don Bosco Oysterbay.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Ufundi na Mashindano wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Nchini (TBF) Manase Zablon amesema kuwa michuano hii imeweza kuonyesha njia kwa wachezaji ambapo katika msimi uliopita wapo wachezaji waliofanikiwa kupata timu na wengine wakipata nafasi za kusoma kupitia mchezo huo.

Kwa mara ya kwanza mashindano ya Sprite Bball Kings yalifanyika 2017 na timu ya Mchenga Bball Stars iliweza kuwa bingwa na kufanikiwa kupata fedha taslimu shilingi million 10 pamoja na Kikombe, Mshindi wa pili wa mashindano alipata shilingi milioni 3 na Mchezaji bora (MVP) Rwehabura Munyangi aka Barongo ambaye alipata kikombe na fedha taslimu shilingi milioni 2.
Mkuu wa Vipindi wa EA Redio Nasa Kingu akizungumza na wawakilishi wa timu za Flying Dribllers na Mchenga BBall Stars pamoja na waandishi wa habari kuelekea fainali ya Michuano ya Sprite BBall Kings 2018 mchezo utakaoanza kutimi vumbi Agosti 18 mwaka huu katika Viwanja vya Ndani wa Taifa. Kulia ni Mkurugenzi wa Ufundi na Mashindano wa Shirikisho la Kikapu Tanzania (TBF) Manase Zablon.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...