Na Robert Hokororo, Ofisi ya Mkurugenzi

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2018, Charles Kabeho ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kwa kutekeleza miradi ya maendeleo yenye ubora na kwa gharama nafuu.

Pia ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutoa fedha kwa ajili ya uimarishaji wa vituo mbalimbali vya afya pamoja na sekta ya elimu.Kabeho ametoa pongezi hizo jana kwa nyakati tofauti wakati akikagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya mendeleo wilayani humo ambako Mwenge wa Uhuru ulikimbizwa.

Sanjari na hilo Kiongozi huyo alipongeza wilaya hiyo kwa kuishirikisha jamii katika kutekeleza miradi hiyo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya elimu na afya jambo ambalo linachangia uboreshaji wa sekta hizo.“Kishapu mna kitu cha pekee tofauti na huko kwengine nilikopita, hapa ninyi katika miradi yenu mlipopewa fedha ndani ya gharama mmebakiza chenji na mnaongeza miradi mingine kwa fedha hizo hizo hivyo mnafanya kitu cha kuigwa,” alisema.

Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge aliongeza kuwa kwa kuishirikisha jamii katika utekelezaji wa miradi hali inayoifanya nayo ifanye uwekezaji wa maendeleo katika senkta mbalimbali.Mwenge wa Uhuru wenye ujumbe “Elimu ni Ufunguo wa Maisha, Wekeza Sasa kwa maendeleo ya Taifa letu” ulikabibidhiwa mkoani Shinyanga wilayani Kishapu ukitokea wilayani Maswa mkoani Shinyanga umepitia miradi ya sh.bilioni 2.2.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2018, Charles Kabeho akizindua mradi wa vyumba vitatu vya madarasa Shule ya msingi Wishiteleja wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Nyabaganga Taraba.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru, Charles Kabeho akiwa ndani ya chumba cha darasa cha Shule ya sekondari Maganzo ambao ni mradi wenye thamani ya sh. miloni 141 uliogharamiwa na fedha kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA). 
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Charles Kabeho akikagua moja ya vyumba vya madarasa Shule ya msingi Wishiteleja wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo
Mwenge wa Uhuru ukikimbizwa katika maeneo mbalimbali wilayani Kishapu ambako ulikagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani sh. bilioni 2.2.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...