Na. Georgina Misama - MAELEZO

Halmashauri zote nchini zimetakiwa kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya Vijana kuyatumia katika shughuli za kilimo.

Wito huo umetolewa leo Jijini Dodoma na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Antony Mavunde wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu maadhisho ya siku ya Vijana Duniani.

Mavunde alisema hadi hivi sasa Serikali imetenga takribani hekta laki mbili katika maeneo mbalimbali nchini ili kuwapa vijana fursa ya kuyatumia katika shughuli za kilimo."Nazitaka Halmashauri zote nchini ambazo bado hazijatenga maeneo hayo, kufanya hivyo ili kuendana na kauli mbiu ya mwaka 2018 inayosema 'Mazingira salama kwa Vijana' ambapo serikali ina wajibu wa kuandaa mazingira hayo kwa vijana." alisema Mavunde.

Akiongelea kuhusu mwitikio wa vijana kwenye shughuli za kilimo, Mavunde alisema kuwa vijana wengi wameanza kujishughulisha katika kilimo na ipo mifano mingi hai ya vijana walioamua kujiajiri kwenye kilimo biashara kama SUGEKO na wanafanya vizuri.

Wakati huo huo Mhe. Mavunde amesema kuwa, Agosti 11 litafanyika kongamano kubwa la Vijana na Wadau wa Maendeleo ya Vijana katika Ukumbi Wa Mikutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mgeni rasmi katika kongamano hilo anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo.KUSOMA ZAIDI  BOFYA HAPA>>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...