Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amewataka viongozi wa Halmashauri nchini kusimamia matumizi ya mapato yanayokusanywa katika Halmashauri zao.

Jafo ametoa kauli hiyo alipokuwa katika ukaguzi wa miradi ya maendeleo wilayani Geita na Chato katika mkoani wa Geita. Amesema Halmashauri mbalimbali zinatakiwa kusimamia vyema matumizi ya mapato hayo na kwa kiasi kikubwa yaelekezwe katika miradi ya maendeleo kwenye Halmashauri hizo kwa maslahi mapana ya wananchi.

Waziri Jafo amepongeza viongozi wa Halmashauri ya Mji wa Geita kwa usimamizi mzuri wa ukusanyaji wa mapato.Katika ziara hiyo, Waziri huyo amefanikiwa kukagua ujenzi wa soko la kisasa linalojengwa kwa fedha za ndani za Halmashauri ya mji wa Geita, barabara za lami za mji wa Geita zinazojengwa kwa mradi wa ULGSP, zahanati ya Buselesele, Kituo cha Afya Bwanga kilichopo wilayani Chato, pamoja na kutembelea shule ya sekondari Magufuli.

Akiwa Buselesele, Waziri Jafo amewahakikishia wananchi wa kata ya Buselesele kwamba serikali itajitahidi ili ijenge kituo cha afya cha kisasa katika kata hiyo ya Buselesele kutokana na idadi kubwa ya wananchi katika eneo hilo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akipata maelezo ya ujenzi wa soko kutoka kwa Mkurugenzi wa mji wa Geita
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Magufuli walipotembelewa leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo
Mkuu wa Mkoa na Geita Mhandisi Robert Gabriel akimueleza jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo alipotembelea katika zahanati ya Buselesele.
Wananchi katika kituo cha afya Bwanga wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...