Mkuu wa maandalizi ya kongamano la kimataifa la Karate chama cha Jundokan, mtindo wa Okinawa Goju Ryu Sensei Dr. Friedrich Gsodam mwenye 9 Dan toka mji wa Vienna, Austria ametuma barua ya kuialika Jundokan tawi la Tanzania.
Uthibitisho wa mwaliko huo ulipokelewa kupitia mkuu wa chama hicho tawi la Tanzania, sensei Fundi Rumadha mwenye Dan 4, na mwalimu mwenye kutambuliwa na chama hicho huko Okinawa, Japan.
 " European Jundokan Gasshuku", linategemewa kufanyika mwezi Julai 19 hadi 21 litawakusanya walimu wote wa chama cha Jundokan toka Okinawa, Japan na nchi za ulaya zote.
Pia, mwenyekiti wa chama hicho Sensei Kancho Miyazato na walimu wakuu walio kuwa naidhini ya ufundishaji wa semina toka chama kijulikanacho kama "Okinawan Budokan", ni sensei Tsuneo Kinjo dan 9, Tetsu Gima, dan 9 na kadhalika.
Tanzania ni nchi pekee katika Afrika mashariki kuwa chini ya Jundokan. Pia vilevile, ikiwa imesalia miezi miwili na nusu kwa maadhimisho ya kusheherekea miaka 65 tangu chama hicho kimeanzishea ambayo itafanikiwa huko kisiwa cha Okinawa.

Sensei Dr.Friedrich Gsodam dan 9 kushoto na sensei Gabriella wa Austria kulia, na sensei Fundi kati.
Masensei wa Jundokan Austria chini ya mkuu wake Sensei Dr. Friedrich Gsodam, kulia.
Sensei Dr. Friedrich Gsodam dan 9 mkuu wa Jundokan Austria kushoto na mwnyekiti wa Jundokan duniani sensei Kancho Miyazato kulia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...